MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Fernando Torres ni miongoni mwa wachezaji wanane wa Ligi Kuu ya England walioteuliwa kwenye kikosi cha Hispania cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, mshambuliaji wa Spurs Roberto Soldado, ambaye amefunga boa moja tu Ligi Kuu England msimu huh ametemwa.
Kopcha wa Hispania, Vicente Del Bosque amemjumuisha kipa wa Manchester United, David De Gea na kiungo wa timu hiyo, Juan Mata, sambamba na Cesar Azpilicueta wa Chelsea, Santi Cazorla wa Arsenal na nyota watatu wa Manchester City, David Silva, Jesus Navas na Alvaro Negredo.
Kikosi kamili cha Hispania ni makipa; Casillas, Reina na De Gea, mabeki; Ramos, Pique, Albiol, Martinez, Juanfran, Alba, Azpilicueta, Carvajal na Moreno.
Viungo ni; Xavi, Xabi Alonso, Iniesta, Koke, Busquets, Cazorla, Iturraspe, Fabregas, Thiago, Mata na Silva wakati
washambuliaji ni; Pedro, Navas, Diego Costa, Villa, Torres, Negredo na Llorente.
0 comments:
Post a Comment