// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MISS TANGA 2014 KUONDOKA NA TOYOTA VITZ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MISS TANGA 2014 KUONDOKA NA TOYOTA VITZ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    MISS TANGA 2014 KUONDOKA NA TOYOTA VITZ

    Na Renatus Mahima, DAR ES SALAAM  
    SAFARI ya kumsaka mrembo wa Tanga 'Miss Tanga 2014' imezinduliwa rasmi huku wadhamini wakuu wa kinyang'anyiro hicho, Nice&Lovely wakitangaza kutoa zawadi ya gari ndogo aina ya Toyota Vitz yenye thamani ya Sh. milioni 10 kwa mshindi.
    Regina Gwae, msemaji wa kamati ya maandalizi ya shindano hilo, katika uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam leo mchana, amesema taji la Miss Tanga 2014 litakabidhiwa kwa mrembo atakayeibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika kwenye ukumbi wa Mkonge Hoteli iliyopo mjini Tanga Juni 21.

    Meneja Mauzo wa Loreal, wanaomiliki bidhaa za Nice & Lovely, Bryan Kelly (kulia) na msemaji wa kamati ya maandalizi ya shindano la Miss Tanga 2014 wakionyesha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo zawadi ya gari litakalokabidhiwa kwa mshindi wa taji hilo.

    "Tumejinga vyema kuhakikisha tunampata mrembo mwenye vigezo atakayeuwakilisha vyema mkoa wa Tanga katika Kanda ya Kaskazini na baadaye kuwania taji la Miss Tanzania," amesema Regina.
    "Mbali na zawadi kubwa ya gari, kuna zawadi nyingine nyingi za fedha taslim kwa washindi wengine ambazo zitatangazwa baadaye," amesema.
    Aliendelea kueleza kuwa fomu za kushiriki zinaendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali mjini Tanga zikiwamo ofizi za The Guardian zilizopo barabara ya 15 na warembo wataingia kambini Tanga Beach Resort jijini Tanga kuanzia Juni 9 hadi Juni 20.
    Bryan Kelly, Meneja Mauzo wa Loreal, wanaomiliki bidhaa za Nice & Lovely, amewashukuru waandaji wa shindano hilo kwa kuwapa nafasi ya kulidhamini.
    Wadhamini wengine wa shindano hilo ni pamoja na vituo vya EATV, East Afrika Radio, Redds, Breeze FM na Mwambao FM.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MISS TANGA 2014 KUONDOKA NA TOYOTA VITZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top