// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); POLISI ZENJI WAENDA SUDAN KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA YA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE POLISI ZENJI WAENDA SUDAN KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA YA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    POLISI ZENJI WAENDA SUDAN KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA YA CECAFA

    Na Ameir Khalid, Zanzibar
    KIKOSI cha wachezaji 18 na viongozi sita wa timu ya Polisi Zanzibar, kimeondoka jana kwenda Sudan kushiriki michuano ya Nile Basin, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
    Timu hiyo iliagwa juzi na kukabidhiwa bendera na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idrisa Muslih Hijja katika makao makuu ya Polisi Ziwani. 
    Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Kamishna na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo, Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wachezaji kuzingatia nidhamu na kufuata maelekezo ya viongozi wao.

    MKUU wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk. Idrissa Muslih Hijja, akimkabidhi bendera ya Zanzibar nahodha wa timu ya Polisi SC Juma Ali Mgunda katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, kabla kikosi hicho kuondoka jana kwenda Sudan kushiriki mashindano ya Nile Basin yanayoandaliwa na Cecafa. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame. (Picha na Ameir Khalid).


    Alisema, Zanzibar ni nchi inayosifika duniani kote kwa nidhamu nzuri, kwa hivyo ni vyema wachezaji hao wakaendeleze sifa hizo kwa muda wote watakapokuwa katika mashindano hayo nchini Sudan.
    "Mkiwa huko mulijue lengo linalokupelekeni Sudan ambalo nina hakika ni kushinda na kurudi na kombe, lakini mjue bila ya nidhamu hamuwezi kutimiza dhamira hiyo," alisema.
    Akizungumza katika hafla hiyo, Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame,  aliwataka wachezaji hao kuthamini nafasi  waliyoipata kwa kucheza kwa kujiamini na kuwa na nidhamu muda wote wa mashindano.
    Kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa timu hiyo Juma Ali Mgunda aliahidi kuwa wanakwenda Sudan kwa ajili ya kushindana na sio kushiriki wakiwa na dhamira ya kufanya vyema na kurudi nyumbani na ubingwa.
    Wachezaji wanaoondoka na timu hiyo ni; walinda mlango, Nassir Suleiman na Sishughuliki Ramadhani, mabeki ni Juma Mgunda, Mohammed Hassan, Suleiman Ali, Abdalla Mwalimu, Mwinyi Ali na Mohammed O. Mmanga.
    Viungo ni Ismail Khamis, Sadiq Ali, Ameir Adam na Ali Anjar, wakati washambuliaji ni Abdalla Omar, Khamis Abdulrahman, Mohammed Seif na Haule Innoccent.
    Viongozi wanaoambatana na kikosi hicho ni kocha mkuu Ali Suleiman Mtuli, msaidizi wake Mohammed Abass, mkuu wa msafara Mohammed Mweri, John Gabriel (Katibu), daktari Mohammed Said na meneja wa timu, Khamis Sadiq.
    Maafande hao wanatarajia kuanza kampeni za kuwania ubingwa wa ngarambe hizo kesho saa 2:00 usiku kwa kupepetana na wenyeji Al Marrekh katika uwanja wa Khartoum.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: POLISI ZENJI WAENDA SUDAN KUSHIRIKI MICHUANO MIPYA YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top