• HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    SUAREZ AINUKA KITANDANI NA KUSEMA; "NITAPAMBANA"

    RATIBA YA URUGUAY

    Juni 14: Vs Costa Rica, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Castelao
    Juni 19: Vs England, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Sao Paulo
    Juni 24: Vs Italia, Saa 11:00 Jioni, Uwanja wa Das Dunas
    MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameshukuru kwa sapoti anayopewa katika wakati huu mgumu na amesema ana matumaini ya kuwa fiti haraka na kurejea uwanjani.
    “Asanteni wote kwa sapoti yenu,’ amesema Suarez akihojiwa na gazeti la La Ovacion la nchini mwao Uruguay.
    “Nitafanya kazi kimya kimya na kwa juhudi katika siku zijazo ili kuwa fiti asilimia 100 ili niweze kuwasaidia wachezaji wenzangu,”.
    Asanteni wote; Luis Suarez akitoka hospitali nchini Uruguay baada ya kufanyiwa upasuaji leo

    Suarez amefanyiwa upasuaji wa goti leo na anatarajiwa kupona ndani ya muda na kucheza Fainali za Kombe la Duni, amesema mama yake. 
    Sandra Diaz amesema upasuaji umefanyika kwa mafanikio na mwanawe anatarajiwa kupona ndani ya wiki tatu, ambayo inamaanisha atauwahi mchezo dhidi ya England Juni 19, mwaka huu. 
    "Upasuaji umemalizika na tunamshukuru Mungu kila kitu kimekwenda vizuri. Matatizo yaliyokuwa yanamsumbua Luis hayakuwa makubwa sana ," alisema kuzungumzia majeruhi ya mwanawe.
    Uruguay, ambayo imedai Suarez alipata maumivu hayo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England msimu huu, bado inajiamini atacheza Juni 19Media scrum: Press wait outside the Medica Uruguaya hospital where Suarez is being treated
    Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali via Habari wajiwa nje ya hospital ya Medica Uruguaya ambako Suarez alikwenda kutibiwa
    Hope of a nation: Uruguay's World Cup chances depend heavily on Suarez
    Tumaini la taifa: Nafasi ya Uruguay kufanya vizuri katika Kombe la Dunia inategema na hali ya Suarez
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SUAREZ AINUKA KITANDANI NA KUSEMA; "NITAPAMBANA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top