KLABU ya Manchester United imekubakli kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos na sasa inaelekeza nguvu zake kwa mchezaji mwenzake Arjen Robben.
day la Pauni Milioni 20 kumnunua Kroos lilikubaliwa wakati David Moyes bado yupo kazini Old Trafford na mroithi wake kocha wa zamani wa Bayern, Louis van Gaal, imeelezwa ameruhusu mango uendelee.
Kroos, mwenye umri wa miaka 24, alifundishwa na Van Gaal alipokuwa Bayern na yuko tayati kufanya kazi tena na kocha wake wa zamani.
Anakwenda Manchester: United imekubali kumnunua kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos (katikati)
Yupo kwenye rada: United sasa inaelekeza nguvu zake kwa mchezaji mwingine wa Bayern Munich, Arjen Robben
Mpango kama huo unahamia kwa Robben, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa mwanzoni kusajiliwa na Van Gaal nchini Ujerumani akitokea Real Madrid kwa Pauni Milioni 20 mwaka 2009.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 30 hive karibuni amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu, lakini anatazamiwa kumfurahisha kocha wa timu ya taiga ya Uholanzi, Van Gaal, am,baye atafanya kazi Robben katika Kombe la Dunia.
Inafahamika United imekubali kutoa Pauni Milioni 27 kumnunua beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw na sentahafu wa Borussia Dortmund, Mats Hummels anawaniwa pia na Van Gaal.
0 comments:
Post a Comment