• HABARI MPYA

    Thursday, May 22, 2014

    CRAIG BELLAMY ATUNGIKA DALUGA ZAKE BAADA YA KUCHEZA KLABU KIBAO ENGLAND

    MKONGWE wa Wales, Craig Douglas Bellamy ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 34. 
    Mshambuliaji huyo wa Cardiff amesema leo kwamba mwili wake hauwezi tena mikiki ya soka ya ushindani.
    Uamuzi wa Bellamy unamfanya ahitimishe miaka 17 ya kucheza soka akiwa na klabu ya nyumbani kwao.
    Bellamy alijiunga na Cardiff kwa mkopo na baadaye kusaini Mkataba wa jumla, akitokea Manchester City.
    Mchezo umekwisha: Mshambuliaji wa Cardiff ametangaza kustaafu akiwa na umri wa miaka 34

    Craig Douglas Bellamy aliyezaliwa Julai 13, mwaka 1979 mjini Cardiff na kisoka aliibukia klabu ya Norwich City kabla ya kuhamia Coventry City na baadaye Newcastle United.
    Kutoka hapo alikwenda kucheza kwa mkopo Celtic mwaka 2005 kabla ya kurejea Ligi Kuu ya England badaye mwaka huo kujiunga na Blackburn Rovers, baadaye Liverpool, West Ham United na Manchester City.
    Msimu wa 2010–2011, Bellamy alishika kucheza daraja la kwanza katika klabu yake ya utotoni, Cardiff City, kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu. Alikwenda kucheza klabu yake ya zamani, Liverpool msimu uliofuata, kabla ya kurejea kwa mkataba wa kudumu Cardiff na baadaye akaiongoza Cardiff kupanda Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya karne moja nusu.
    Danger man: Bellamy celebrates scoring against Aston Villa for Manchester City in October, 2009
    Mtu hatari: Bellamy akishangilia bao lake alilofunga dhidi ya Aston Villa wakati akiichezea Manchester City Oktoba mwaka 2009

    Wakati wake akicheza, Bellamy ametwaa mataji ya Championship (Daraja la Kwanza), Kombe la Ligi, Kombe la Scotland na Ngao ya Jamii. Pia alishika nafasi za pili katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa. Amekuwa akishutumiwa kwa tabia zake mbaya ndani na nje ya Uwanja, lakini amekusanya mamilioni ya Pauni kwa shughuli za hisani na pia ameanzisha akademi ya soka nchini Sierra Leone.
    Aliichezea kwa mara ya kwanza Wales mwaka 1998 na miaka 15 baadaye alicheza jumla ya mechi 76 na kufunga mabao 19. Alikuwa nahodha wa Wales kuanzia mwaka 2007 hadi 2011, alipojiuzulu kutokana na majeruhi.
    Return: Bellamy, pictured here celebrating a goal against Manchester City in January 2012, had two spells at Liverpool
    Aliporejea: Bellamy, pichani akishangilia bao aliloifungia Liverpool dhidi ya Manchester City Januari mwaka 2012

    Alistaafu soka ya kimataigfa baada ya mechi za kufuzu za Kombe la Dunia mwaka 2014. Pia alikuwemo kwenye kikosi cha Uingereza kilichoshiriki michezo wa Olimpiki mwaka 2012 mjini London, akicheza mechi tano na kufunga bao moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CRAIG BELLAMY ATUNGIKA DALUGA ZAKE BAADA YA KUCHEZA KLABU KIBAO ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top