KIUNGO wa zamani wa Chelsea, Claude Makelele ataachia nafasi yake ya Ukoha Msaidizi wa PSG ili aka we kocha mpya Mkuu wa timu ya Ligue 1 pia, Bastia.
Makelele, ambaye enzi zake alichezea klabu za Real Madrid, Chelsea na PSG anaweza kutambulishwa kama kocha mpya wa Bastia kabla ya mwishoni mea wiki kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa, L'Equipe.
PSG ilimpa Makelele ofa ya Mkataba wa miaka miwili zaidi, lakini amegoma ili aka we bosi kamili timu nyingine.
Ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Ufaransa, Willy Sagnol kuwa kocha mpya Mkuu katika Ligue 1 baada ya beki huyo wa zamani wa Bayern Munich kuwa mbioni kuteuliwa kocha mpya wa Bordeaux.
Mkali wa enzi hizo: Makelele alikuwa gwiji Stamford Bridge ambako alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu England
Makelele, mwenye umri wa miaka 41, alikuwa chachu ya mafanikio ya mwanzoni ya kocha Mreno Jose Mourinho Stamford Bridge.
Akiwa amesajiliwa kutoka Real Madrid mwaka 2003, Makelele alikuwa mchezaji muhimu mno katika mfumo wa Mourinho wa 4-3-3, akiwafanya watu Frank Lampard kufunga sana mabao.
0 comments:
Post a Comment