• HABARI MPYA

    Tuesday, May 13, 2014

    RIO FERDINAND ALIVYOTEMWA 'KIROHO MBAYA' MAN UNITED

    BEKI Rio Ferdinand amemaliza maisha take ya soka Manchester United baada ya kuambiwa hatapewa Mkataba mpya.
    Mkuu wa Old Trafford, Ed Woodward alimpa habari hizo za kusikitisha Ferdinand mwenye umri wa miaka 35 katika chumba cha kubadilishia nguo Jumapili wakati wa mchezo wa mwisho na Southampton. 
    Wengi wamesikitishwa na kitendo cha Woodward kuamua kumuacha 'kiroho mbaya' Ferdinand baada ya miaka 12 ya kuitumikia klabu hiyo kwa moyo wake wote.

    Anaondoka: Rio Ferdinand anaondoka Manchester United kama mchezaji baada ya klabu kukataa kumuongezea Mkataba
    Champions: Ferdinand shows off the 2006/07 Premier League trophy with Cristiano Ronaldo
    Kumbukumbu za furaha: Ferdinand akiwa ameshika taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2008 na Cristiano Ronaldo baada ya kuifunga Chelsea kwa penalti
    New boy: Ferdinand shows off his United shirt with then manager Sir Alex Ferguson after joining from Leeds for £29.1million in July, 2002
    Alipowasili: Ferdinand akikabidhiwa jezi ya United na mocha wakati huo, Sir Alex Ferguson baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea Leeds kwa dau la uhamisho la Pauni Milioni 29.1 Julai mwaka 2002

    FERDINAND MAN UNITED

    Kusajiliwa: July 2, 2002
    Ada: Pauni Milioni 29.1
    Mechi alizocheza: 455
    Mabao aliyofunga: 8
    Mataji aliyoshinda: Ligi Kuu (2002/03, 2006/07, 2007/08, 2008/09, 2010/11, 2012/13), Ligi ya Mabingwa (2007/08), Kombe la Ligi (2005/06, 2008/09), Kombe la Dunia la Klabu (2008)
    Katika taarifa aliyoweka kwenye tovuti yake binafsi usiku wa jana, Ferdinand amesema; "Mambo fulani yamenifanya nishindwe kusema kwaheri kwa namna amabyo ningependa,".
    Na huku akiwa amekubali kumruhusu beki mwingine wa kati Nemanja Vidic kuondoka, mchezaji mwenzake wa zamani Ferdinand, Gary Neville ametweet: "Hivyo inaonekana kama Rio na Vida wameruhusiwa kuondoka!!!
    Beki huyo wa zamani wa England amewaambia wenzake safe ya 1-1 juzi ndiyo ilikuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo wakiwa kwenye ndege kurejea kutoka St Mary na akawaomba wamsainie mpira abaki nao kama kumbukumbu yake.
    Ferdinand, ambaye alikuwa mchezaji ghali kihistoria England wakati anasajiliwa United kutoka Leeds kwa dau la Pauni Milioni 29.1 Julai mwaka 2002, ameichezea timu hiyo mechi 455 lakini alionekana hafai chini ya David Moyes.
    Hard man: Ferdinand is escorted from the pitch by Robin van Persie after being cut by a coin thrown from the crowd during a Manchester derby in 2012
    Amemwaga damu: Ferdinand akisindikizwa kutoka uwanjani na Robin van Persie baada ya kuchanwa na sarafu iliyorushwa uwanjani na mashabiki wakati wa mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester mwaka 2012
    On target: Ferdinand scores a rare goal against Liverpool in a 2-0 win at Old Trafford in 2006
    Alikuwa anafunga pia: Ferdinand akifunga boa dhidi ya Liverpool katika ushindi wa 2-0 Uwanja wa Old Trafford mwaka 2006

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RIO FERDINAND ALIVYOTEMWA 'KIROHO MBAYA' MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top