• HABARI MPYA

    Tuesday, May 13, 2014

    BRENDEN RODGERS AIFUTA CHOZI LIVERPOOL KWA TUZO YA LMA

    KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers ameshinda tuzo ya LMA ya Kocha Bora wa Mwaka katika sherehe zilizofanyika jana usiku, na kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa klabu hiyo kushinda tuzo hiyo.
    Mwalimu huyo wa Wekundu wa Anfield alikuwa na msimu mzuri akiiongoza timu hiyo ya Merseyside kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi kwa Luis Suarez na wenzake kulikosa Kombe siku ya mwisho kabisa walipopigwa na Manchester City.
    Kocha wa England, Roy Hodgson ndiye alimkabidhi tuzo hiyo mocha huyo mwenye umri wa miaka 41, ambayo hutokana na kura zinazopigwa na makocha wa maharaja tote manne.
    Bora zaidi: Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers ameshinda tuzo ya LMA ya Kocha Bora wa Mwaka jana usikuNight to remember: Rodgers was presented with the award by England manager Roy Hodgson (left)
    Usiku wa kukumbukwa: Rodgers akikabidhiwa tuzo hiyo na kocha wa England, Roy Hodgson (kushoto)

    WASHINDI WA TUZO ZA LMA;

    Kocha Bora wa Mwaka wa LMA; imedhaminiwa na Barclays
    Brendan Rodgers, Liverpool – alikabidhiwa na Roy Hodgson
    Tuzo Maalum ya LMA;
    Russ Wilcox, Scunthorpe United – ilikabidhiwa na Sir Alex Ferguson CBE
    Tuzo ya Kazi za Soka LMA;
    Norman Rimmington, Barnsley – ilikabidhiwa na Danny Wilson
    Kocha Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Barclays;
    Tony Pulis, Crystal Palace - ilikabidhiwa na Howard Wilkinson
    Sky Bet Football League Championship Manager of the Year 
    Nigel Pearson, Leicester City – presented by David Moyes
    Sky Bet Football League 1 Joint Managers of the Year
    Kenny Jackett, Wolves & Russell Slade, Leyton Orient – presented by Sam Allardyce
    Kocha Bora wa Ligi Daraja la Pili;
    Russ Wilcox, Scunthorpe United – ilikabidhiwa na Chris Hughton
    Kocha Bora wa Kombe la FA;
    Nigel Clough, Sheffield United – ilikabidhiwa na Roberto Martinez
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRENDEN RODGERS AIFUTA CHOZI LIVERPOOL KWA TUZO YA LMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top