• HABARI MPYA

    Monday, May 12, 2014

    ENGLAND YATAJA ASKARI 23 WA KOMBE LA DUNIA

    KOCHA Roy Hodgson amefichua kikosi cha wachezaji 23 wa England, Three Lions kitakachokwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil baadaye mwezi huu.
    Hodgson amethibitisha atabeba na makinda wa akiba kwenda kwenye fainali hizo kujaribu kumaliza ukame wa England kucheza Kombe la Dunia miaka 48 bila kushinda taji.
    Kikosi hicho ni makipa; Joe Hart, Fraser Forster na Ben Foster, mabeki; Gary Cahill, Phil Jagielka, Chris Smalling, Phil Jones, Glen Johnson, Leighton Baines na Luke Shaw, wakati viungo ni Steven Gerrard, James Milner, Jack Wilshere, Ross Barkley, Alex Oxlade-Chamberlain, Jordan Henderson, Raheem Sterling, Adam Lallana na Frank Lampard wakati washambuliaji ni Daniel Sturridge, Wayne Rooney, Danny Welbeck na Rickie Lambert.


    THe boss: Roy Hodgson has named his 23 man squad for the World Cup in Brazil
    Bosi kubwa: Kocha Roy Hodgson ametaja kikosi cha wachezaji 23 wa Kombe la Dunia
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ENGLAND YATAJA ASKARI 23 WA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top