// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY YAPANGWA KUNDI SI MCHEZO MICHUANO MIPYA YA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY YAPANGWA KUNDI SI MCHEZO MICHUANO MIPYA YA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 12, 2014

    MBEYA CITY YAPANGWA KUNDI SI MCHEZO MICHUANO MIPYA YA CECAFA

    Na Princess Asia, Dar es Salaam
    MBEYA City imepangwa kundi B katika michuano maalumu ijulikanayo kama Nile Basin itakayopigwa  Sudan kuanzia Mei 22 hadi Juni 2.
    Katika droo ya michuano hiyo inayoshirikisha washindi wa pili na mabingwa wa Kombe la FA wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), iliyopangwa leo, Mbeya City iliyopewa nafasi ya Azam iliyojitoa imepangwa Kundi B pamoja na timu za AFC Leopards ya Kenya),  El Merreikh Al Fasher ya Sudan na  Elman ya Somalia. 
    Kikosi cha Mbeya City ambacho kitashiriki michuano mipya ya CECAFA

    Kundi A lina na timu za El Merreikh ya Sudan, 
    Victoria University ya Uganda, Malakia ya Sudan
    Kusini na Polisi ya Zanzibar, wakati Kundi C linaundwa na Al Ahli Shandi ya Sudan, Al Masry ya Misri, Defence ya Ethiopia na  Dkhill  ya Djibouti na 
    Kundi D lina timu za Hey Al Arab ya Sudan, Arab
    Contractors ya Misri, Flambeau ya Burundi na Etincelles ya Rwanda.
    Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amezungumzia droo hiyo na kusema wamepangwa kundi gumu, lakini watajipanga ili waweze kufanya vizuri. Amesema anafurahi ratiba wameipata mapema, itawasaidia kujipanga mapema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAPANGWA KUNDI SI MCHEZO MICHUANO MIPYA YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top