MWANASOKA Bora wa Mwaka wa Chelsea ni Eden Hazard, aliyeshinda tuzo hiyo na kukabidhiwa jana.
Kiungo guti wa Ubelgiji alikuwa na msimu mzuri chini ya kocha Jose Mourinho, akifunga mabao 14 na kumaliza kama mfungaji bora wa klabu.
Hazard, aliyetua Stamford Bridge akitokea Lille mwaka 2012, pia msimu huh ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora Chipukizi wa PFA, aliyokabidhiwa mwezi uliopita baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya nyota wa Liverpool, Luis Suarez aliyeshinda.
Nyota kweli: Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akimkabidhi Eden Hazard tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa klabu hiyo
Pamoja na mabao hayo aliyofunga, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alitoa pasi za mabao saba kuisaidia The Blues kumaliza katika nafasi ya taut kwenye Ligi Kuu ya England na kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mchezaji huyo aliyeripotiwa kutakiwa na Paris Saint-Germain alikuwa akikandiwa na Mourinho wiki za karibuni, lakini Special One ameonyesha hana kinyongo naye kwa kumkabidhi Hazard tuzo hiyo.
Cesar Azpilicueta ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Wachezaji wa Mwaka baada ya kushinda jura za wachezaji wenzake tang aanze kucheza kikosi cha kwanza Novemba.
Mspanyola huyo aliyempokonya namnba Ashley Cole tang wakati huo amekuwa beki wa kushoto chaguo la kwanza.
Chaguo la wachezaji: Beki Cesar Azpilicueta (katikati) akiwa amepozi na tuzo yake kwa pamoja na kipa wa zamani wa Chelsea, Carlo Cudicini (kushoto)
Gwiji: Beki wa zamani wa Chelsea, Paulo Ferreira akipokea tuzo maalum ya kutambuliwa kwa mchango wake kutoka kwa Lord Sebastian Coe
Kifaa cha baadaye: Kinda Lewis Baker ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora chipukizi wa Mwaka
0 comments:
Post a Comment