• HABARI MPYA

    Thursday, June 18, 2026

    GHANA YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA, YAILAZA PANAMA 1-0 CANADA


    TIMU ya Ghana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama katika mchezo wa Kundi L Fainali za Kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo Uwanja wa BMO Field, Toronto nchini Canada.
    Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo chipukizi wa umri wa miaka 20 anayechezea klabu ya Nordsjælland ya nchini Denmark, Caleb Marfo Yirenkyi aliyefunga dakika ya 90’+5. 
    Mchezo mwingine wa kundi hilo uliotangulia usiku wa kuamkia leo England imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia Uwanja wa AT&T Stadium, Arlington, Texas, Marekani.
    Mabao ya Three Lions yamefungwa na Nahodha na mshambuliaji, Harry Edward Kane wa Bayern Munich ya Ujerumani mawili, dakika ya 12 kwa penalti na dakika ya 42, kiungo wa Real Madrid ya Hispania, Jude Victor William Bellingham dakika ya 47 na mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford anayecheza kwa mkopo Barcelona ya Hispania dakika ya 85.
    Kwa upande wao Croatia, mabao yao yamefungwa na kiungo wa Como ya Italia, Martin Baturina mzaliwa wa Uswisi dakika ya 36 na mshambuliaji wa FC Dallas ya Marekani, Petar Musa dakika ya 45+5.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GHANA YAANZA VYEMA KOMBE LA DUNIA, YAILAZA PANAMA 1-0 CANADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top