• HABARI MPYA

  Sunday, September 16, 2018

  MBEYA CITY YAZINDUKIA KWA VIBONDE ALLIANCE FC YA MWANZA, YAWACHAPA 2-0 SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  TIMU ya Mbeya City imepata ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya kandanda Tanzania Bara kufuatia kuichapa 2-0 Alliance FC ya Mwanza mchana wa leo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Ushindi huo umetokana na bao moja la kipindi, Victor Hangaya akianza kufunga la kwanza dakika ya 18 kabla ya Eliud Ambokile kufunga la pili dakika ya 81.
  Ushindi huo unaifanya Mbeya City iokote pointi tatu za kwanza baada ya kufungwa mechi tatu mfululizo zilizopita zote ugenini, 2-0 mara mbili na Azam FC na Simba SC na 2-1 Manungu kwa Mtibwa Sugar.

  Kwa Alliance FC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu, inafikisha mechi ya nne bila ushindi ikiwa na pointi moja tu iliyovuna kwenye sare moja ya 1-1 nyumbani na African Lyon huku mechi nyingine mbili ikifungwa pia 1-0 na Mbao FC mjini Mwanza na 2-0 na Tanzania Prisons mjini Mbeya pia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAZINDUKIA KWA VIBONDE ALLIANCE FC YA MWANZA, YAWACHAPA 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top