• HABARI MPYA

    Tuesday, September 04, 2018

    KUSHUHUDIA MECHI ZA BUNDESLIGA NI SH 13,000 TU NDANI YA STAR TIMES

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia king’amuzi chake cha StarTimes imetangaza kurejea kwa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga msimu wa 2018/19. Taarifa hii imetolewa leo jumanne na Meneja Masoko wa kampuni hiyo Bw. David Malisa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye duka la StarTimes Bamaga.
    Ligi ya Ujerumani ni miongoni mwa ligi kubwa na bora kabisa barani ulaya, ikiwa na wachezaji mahiri kama mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Lewandowski, Marco Reus, mjamaica Leon Bailey na wengine wengi. Katika msimu huu wa 2018/19 StarTimes wamezidi kuinogesha Bundesliga kwani itakuwa ikitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.
    “Ikumbukwe kwamba StarTimes pekee ndio tunaonyesha ligi ya Bundesliga na sasa burudani inaongezeka maradufu kwa sababu mechi zitatangazwa kwa lugha yetu ya nyumbani yaani Kiswahili, na wachambuzi makini kabisa wenye weledi katika soka la ulaya. Pia mechi zote zitakuwa zikipatikana kwa kiwango cha HD kwenye chaneli zetu za Michezo”.
    Meneja Masoko Stars Times, David Malisa (kushoto) akiwa na Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Zamaradi Nzowa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam 
    Zamaradi Nzowa akiwa na wasanii mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Bundesliga leo

    Mbali na ligi ya Bundesliga, StarTimes pia ni warushaji wa ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambayo ina mastaa kama Neymar na kinda machachari Kylian Mbappe. Ligue 1 ambayo imeanza takribani wiki mbili zilizopita inasifika sana kwa kuwa chimbuko la vipaji vingi ambavyo vinatamba katika ligi mbalimbali, hivyo ni burudani ya aina yake kwa wateja wa StarTimes wanaopenda kandanda.
    “Mechi zote za Bundesliga na zile za Ligue 1 zinapatikana kuanzia kifurushi cha MAMBO kwa Tsh 13,000/= tu kwa watumiaji wa visimbusi vya Antenna na kifurushi cha SMART Tsh 19,000/= kwa watumiaji wa visimbusi vya Dish, kupitia chaneli zetu za michezo yaani World Football, Sports Premium, Sport Focus ambazo zote zinapatikana kwa kiwango cha HD. Hivyo wateja wetu wana uhakika wa kufurahia picha safi zaidi wanapokuwa wakitazama kandanda la Bundesliga na Ligue 1” aliongezea Malisa
    Kwa upande wake Meneja Maudhui wa StarTimes Bi. Zamaradi Nzowa aliwatambulisha mastaa kadhaa ambao watafanya nao kazi katika kuhakikisha taarifa zinafika kwa wakati kwa wateja ambao muda mwingi wanakuwa katika mitandao ya kijamii. Aliwatambulisha Madee, Dogo Janja, Mkali wenu, luninga ya mtandaoni Shuti Kali na Ukurasa wa michezo wa Worldsport14.
    Kuhusu StarTimes
    StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KUSHUHUDIA MECHI ZA BUNDESLIGA NI SH 13,000 TU NDANI YA STAR TIMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top