• HABARI MPYA

    Monday, May 12, 2014

    STARS NA ZIMBABWE YARUDISHWA DAR, KUCHEZWA JUMAPILI TAIFA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    MECHI ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania, Taifa Stars na Zimbabwe, Mighty Warriors itafanyika Jumapili Mei 18, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Awali mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
    Basi la Taifa Stars litaingiza timu Uwanja wa Taifa Jumapili
    Ili Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye Uwanja huo Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.
    “Tunatoa mwito kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA),”imesema taarifa ya TFF.
    Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS NA ZIMBABWE YARUDISHWA DAR, KUCHEZWA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top