Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BEKI aliyekuwa akitajwa kuwania na Azam FC, Mbuyu Junior Twite leo ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Yanga SC ya Dar es Salaam.
Tovuti ya Yanga SC imeandika kwamba hatua hiyo inakuja baada ya Twite kufikia makubaliano na uongozi na kupata majibu ya Shirikisho la Soka nchini TFF juu ya idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa msimu ujao 2014/2015.
Usajili wa Twite umefanyika leo makao makuu ya klabu ya Yanga chini ya Katibu Mkuu Bw Beno Njovu ambapo mchezaji amesema ataendelea kujitolea kwa uwezo wake kuisaidia timu yake ya Yanga.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na beki huyo wa Rwanda mwenye asili ya DRC, baada ya pande zote kukubaliana, hivyo kuanzia sasa Twite ataendelea kuwa mchezaji wetu kwa msimu ujao wa 2014/2015 na kusisitiza kuwa usajili ndio umeanza sasa.
Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio.
Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Yanga SC kwa kipindi cha miaka miwili tangu Julai 2012 aliposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.
Hivi karibuni, Azam FC ilisajili wachezaji wawili mfululizo waliokuwa wamemaliza mikataba yao Yanga SC, ambao ni kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu na jana Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji alisema baada ya pigo hilo atasajili wachezaji wengine bora.

![]() |
| Anabaki; Mbuyu Twite akiwa ameshika jezi ya Yanga SC baada ya kusaini Mkataba wa awali wakati anajiunga na klabu hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Abdallah Ahmed Bin Kleb. |
Akiongea mara baada ya kuweka sahihi kwenye mkataba wake mpya Twite amesema anajisikia furaha kuendelea kuwa mchezaji wa Yanga, kwani anafurahia maisha ya Jangwani, wapenzi, washabiki, viongozi na wachezaji ni marafiki/ndugu ndani na nje ya Uwanja.
Aidha Twite amesema Yanga ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, zenye washabiki na waachama wengi hivyo wangu ni fahari kuendelea kuitumika timu hii ambayo tangu kujiunga nayo nimekua nikijtoa kwa moyo wangu wote kusaka mafanikio.
Mbuyu Twite amekua ni mchezaji wa Yanga SC kwa kipindi cha miaka miwili tangu Julai 2012 aliposajiliwa huku katika kipindi hicho chote akiwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza ambapo msimu uliopita aliweza kuisadia timu yake kutwaa Ubingwa wa Lig Kuu ya Vodacom na msimu huu kushika nafasi ya pili.
Hivi karibuni, Azam FC ilisajili wachezaji wawili mfululizo waliokuwa wamemaliza mikataba yao Yanga SC, ambao ni kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu na jana Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji alisema baada ya pigo hilo atasajili wachezaji wengine bora.

.png)
0 comments:
Post a Comment