Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
KATIKA kile kinachoonekana Yanga imepania kuachana na mshambuliaji wake Emmanuel Okwi, uongozi wa klabu hiyo umempa masharti magumu nyota huyo wa Uganda.
Yussuf Manji, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga amesema jana kwenye makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam kuwa uongozi wake uko katika mazungumzo na Okwi ili afidie muda alioupoteza wakati akisubiri kibali chake cha kuitumikia timu hiyo ya Jangwani au wavunje mkataba naye.
"Tumemsajili Okwi kwa mkataba wa miaka miwili na nusu lakini katika usajili huo gharama zote za kibali cha yeye kucheza mpira nchini ni juu yake mwenyewe," amesema Manji.
"Nyote mnatambua Okwi hajacheza mechi sita za mwanzo, tumemuita tukamwambia inabidi tuongeze muda uliopotea kwenye mkataba wake kmwa sababu robo kwa maana ya asilimia 10 au 20 ya muda wa mkataba wake imepotea hatujapata huduma zake.
"Aje tuzungumze tuongeze muda huo au tupungumze muda arudishe pesa. Hiki ndicho kinachooendelea kati ya Okwi na uongozi wa Yanga na kesho Katibu Mkuu (Beno Njovu) atamwandikia barua kumkumbusha," amesema zaidi Manji.
Aidha, Manji ambaye alikuwa amefura kutokana na baadhi ya viongozi wa matawi hasa tawi la Tandale alilolifutilia mbali kutokana na chokochoko dhidi ya uongozi wake, amesema Yanga haina haraka na Okwi kwa kuwa haikumsajili kwa ajili ya mashindano ya ndani ya mipaka ya Tanzania.
"Sisi hatuna haraka na Okwi, kwa nini ninasema hivyo? Ni kwa sababu tulimsajili kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na si michuano ya ndani ya Tanzania. Kwa hiyo bado tuna muda mzuri wa negotiations (majadiliano) naye," amesema Manji, ambaye katika mkutano huo na waandishi wa habari alikuwa amefuatana na makamu wake Clement Sanga, Njovu, Kaimu Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, viongozi wa Baraza la Wazee la Yanga na Wenyekiti na Makatibu wote wa matawi ya Dar es Salaam isipokuwa tawi la Tandale ambao amewafuta uanachama.
Okwi. mchezaji wa zamani wa Simba na SC Villa ya kwao Uganda, alisajiliwa Yanga siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo msimu huu Desemba 15 mwaka jana baada ya kuikacha timu yake ya Etoile du Sahel (ESS) ya Ligi Kuu ya Tunisia lakini alizuiwa kuichezea Yanga na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kusaka ufafanuzi wa usajili wake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Mkali huyo wa kufumania nyavu aligoma kucheza michezo kadhaa ya mwisho wa msimu wa 2013/14 akitaka uongozi wa Yanga umalizie fungu la zaidi ya Sh. milioni 60 za kusaini mkaba nao.
"Ninaendelea kutoa onyo kwa wanachama na viongozi wa Yanga kuongea ovyo na vyombo vya habari pasipo kufuata utaratibu na katiba ya Yanga. Leo ninafuta tawi la Tandale na hata wakija kuomba tena uanachama wa Yanga mimi sitasaini," amesema.

![]() |
| Yanga SC inatafuta namna ya kuvunja mkataba na Okwi kulia |

.png)
0 comments:
Post a Comment