Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
MAKOCHA wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na
Nigeria (Flying Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari
kuzungumzia mikakati yao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.
Mkutano huo utafanyika kesho (Mei 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa
mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
![]() |
| Kikosi cha Ngorongoro ambacho kitamenyana na Fliying Eagles Jumapili |
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa
10 kamili jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Fainali hizo za 19 za Afrika zitafanyika mwakani nchini Senegal
zikishirikisha timu saba zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na Senegal
wanaoingia moja kwa moja kutokana na kuwa wenyeji.
Wakati Ngorongoro Heroes leo (Mei 9 mwaka huu) saa 10 jioni
itafanya mazoezi yake Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Flying Eagles yenyewe muda
huo huo itafanya mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati
upande wa VIP itakuwa sh. 5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika
magari maalumu.



.png)
0 comments:
Post a Comment