Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inayoshirikisha timu 27 inaanza
kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya
na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi A ambalo mechi za
ke zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro, African Sports ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8
mchana wakati saa 10 jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto
Shooting Stars ya Mtwara.
Jumapili (Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi
kati ya Bulyanhulu FC (Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8
mchana wakati saa 10 jioni ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar
es Salaam.
Kundi B katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
litaanza ligi kwa mechi kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8
mchana wakati saa 10 jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei 11 mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na
Magereza ya Iringa wakati Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe
zitaumana kuanzia saa 10 jioni.
Simiyu United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza
kucheza saa 8 mchana katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga. Saa 10 jioni ni mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa
wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili (Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida
United (Singida) na Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni
pambano kati ya mabingwa wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC
ya Geita.
Ligi hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza
kila kundi itapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa
2014/2015.
0 comments:
Post a Comment