// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); IBRAHIMOVIC MWANASOKA BORA UFARANSA MARA YA PILI MFULULIZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE IBRAHIMOVIC MWANASOKA BORA UFARANSA MARA YA PILI MFULULIZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 12, 2014

    IBRAHIMOVIC MWANASOKA BORA UFARANSA MARA YA PILI MFULULIZO

    MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 kwa mara ya pili mfululizo.
    Ibrahimovic amefunga mabao 25 katika ligi na kuiwezesha PSG kutwaa taji la ligi hiyo ya Ufaransa kwa rekodi ya kufikisha pointi 86 points, sambamba na kufunga mabao 10 katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
    Na Msweden huyo anayezungumza kwa ufasaha lugha tano tofauti za kimataifa, aliwavunja mbavu wachezaji wenzake kwa kuzungumza Kifaransa kibovu. 
    Anajiuma uma: Ibrahimovic akijitahidi kuzungumza Kifaransa wakati wa kutoa hotuba ya kushukuru

    Wakati anazungumza, wachezaji wenzake wa PSG Salvatore Sirigu na Marco Verratti walivunjika mbavu kwa kucheza Kifaransa chake kibovu.
    Lakini alipozungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Ibrahimovic alisema: "Najivunia sana. Inaonyesha kwamba ulikuwa msimu mzuri kwa PSG. Kwangu, pia, labda bora zaidi katika maisha yangu ya soka,".
    Prize winner: Ibrahimovic and his awards
    One, two, three: Ibrahimovic checks out his awards
    Mshindi mkuu: Ibrahimovic akiwa na tuzo zake

    Ibrahimovic pia ameshinda Tuzo ya Bao Bora la Mwaka alilofunga katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Bastia Oktoba mwaka jana.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 pia amewahi kushinda ubingwa wa Uholanzi mara mbili akiwa na Ajax (mwaka 2002 na 2004), Italia maarufu kama Serie A akiwa na Inter Milan mara tatu ( kuanzia 2007 hadj 2009), La Liga akiwa Barcelona (mwaka 2010), na Italia tena akiwa AC Milan (mwaka 2011).
    Pia alishinda mfululizo mataji ya Serie A akiwa na Juventus mwaka 2005 na 2006, lakini mataji hayo walipokonywa kwa kashfa ya cupping matokeo.
    Ibrahimovic atacheza mechi take ya mwisho msimu huu Jumamosi wakati PSG itakapomenyana na Montepllier katika mechi za kufunga msimu na kwa bahati mbaya hatakwenda Brazil kwenye Kombe la Dunia, kA kuwa Sweden haijafuzu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IBRAHIMOVIC MWANASOKA BORA UFARANSA MARA YA PILI MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top