• HABARI MPYA

    Monday, January 07, 2013

    SHIKOKOTI ASEMA KOMBE LA MAPINDUZI NI LA TUSKER TU


    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    NAHODHA wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi, michuano inayoendelea visiwani hapa.
    Akizungumza jana, Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na Azam ni wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe.
    “Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.
    Tusker, mabingwa wa Kenya, jana jioni walikuwa timu ya kwanza kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuilaza Jamhuri ya Pemba bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wake hatari, Jesse Were dakika ya 23 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Ushindi huo, umewafanya wababe hao wa soka ya Kenya wamalize mechi zao za Kundi A wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Simba SC iliyomaliza na pointi tano.
    Jamhuri iliyomaliza na pointi tatu na Bandari ambayo imeambulia pointi moja, zimeaga mashindano haya. Simba na Tusker zinasubiri mechi za leo za mwisho za Kundi B ili kujua wapinzani wao katika Nusu Fainali. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SHIKOKOTI ASEMA KOMBE LA MAPINDUZI NI LA TUSKER TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top