• HABARI MPYA

    Monday, January 07, 2013

    AZAM, COASTAL NA MTIBWA ZAWANIA NUSU FAINALI MAPINDUZI LEO

    Mabingwa watetezi Azam, watafuzu?

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    TIMU mbili zitakazokamilisha idadi ya timu za kucheza hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, zinatarajiwa kujulikana leo, wakati mechi mbili kali zitakapopigwa kwenye viwanja viwili tofauti visiwani hapa leo.
    Coastal Union ya Tanga inayoshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza, itaanza kumenyana na Miembeni kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung saa 10:30 jioni, kabla ya mabingwa watetezi kupambana na mabingwa wa zamani wa michuano hii, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan, kuanzia saa 2:30 usiku wa leo.
    Azam ndio inaongoza Kundi B kwa pointi zake nne, wakifuatiwa na Miembeni wenye pointi tatu, Coastal pointi mbili na Mtibwa yenye pointi moja inashika mkia.
    Iwapo Mtibwa itaifunga Azam na Coastal itatoka sare, timu hiyo ya Manungu itaangaliwa mustakabali wake wa kufuzu Nusu Fainali kwa kulinganishwa wastani wake wa mabao na Miembeni.
    Coastal wakishinda wanaweza kufuzu moja kwa moja hata kama Mtibwa ikiifunga Azam, kwani watafikisha pointi tano.
    Kwa ujumla, hadi sasa timu yoyote kati ya zote nne za Kundi B inaweza kufuzu Nusu Fainali na hii inamaanisha hili ndilo lilikuwa Kundi la kifo.     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM, COASTAL NA MTIBWA ZAWANIA NUSU FAINALI MAPINDUZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top