• HABARI MPYA

    Saturday, January 19, 2013

    AZAM YAPIGWA 2-1 IKISTAHILI KUSHINDA 3-2 KENYA

    Mfungaji wa bao la Azam leo, Samih Hajji Nuhu
     akipongezwa na Mwaikimba

    Na Prince Akbar
    AZAM FC imeanza vibaya ziara yake ya Kenya, baada ya kufungwa mabao 2-1 kwa tabu na wenyeji AFC Leopard katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, jioni hii.
    Mabao ya washindi katika mchezo huo, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la Azam lilifungwa na Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
    Hata hivyo, Azam itabidi wajilaumu wenyewe kupoteza mchezo huo, kwani walipoteza penalti mbili kupitia kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
    Pamoja na kufungwa, Azam ilionyesha soka maridadi jioni ya leo mjini hapa kiasi cha kuwavutia mashabiki wa Kenya, waliojikuta wakiishangilia baada ya kuzimikia soka yao.
    Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, Luckson Kakolaki, Joackins Atudo, Abdulhalim Humud/Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aiziz/Humphrey Mieno, Salum Abubakar/Kipre Balou, Gaudence Mwaikimba/Brian Umony, Khamis Mcha na Uhuru Suleiman/Abdi Kassim ‘Babbi’.

    AFC Leopards: Martin Musalia, Edwin Wafula, Antony Kimani, Eric Masika, Noah Abich, Martin Imbalambala, Patillah Omoto, Bernard Mangoli, Victor Ochieng, Mike Baraza, Paul Were.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: AZAM YAPIGWA 2-1 IKISTAHILI KUSHINDA 3-2 KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top