• HABARI MPYA

    Thursday, May 28, 2026

    TANZANIA YATINGA FAINALI AFCOM U17, YAITOA MISRI KWA MATUTA


    TANZANIA imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17(AFCON U17) baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Misri kufuatia sare ya bila kufungana usiku huu Uwanja wa Moulay El Hassan Jijini Rabat nchini Morocco.
    Pongezi kwa kipa wa Serengeti Boys, Haji Ally Abdallah aliyeokoa mikwaju ya penalti ya Abdullah Amr na Mohamed Nour – huku za Abdelaziz Khaled Shabaan Said, Amir Abu El Ezz na Mohamed Gamal pekee wakifanikiwa kumtungua mlinda mlango huyo hodari wa Tanzania.
    Waliofunga penalti za Tanzania ni Luqman Mbalasalu, Kassim Juma, Idrisa Kilendemo na Erick Yusuph huku ya Razaki Mbegelendi ikiokolewa na kipa wa Mafarao Wadogo, Malik Amr.
    Tanzania sasa inasubiri mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya wenyeji, Morocco na Senegal zinazomenyana muda huu hapo hapo Uwanja wa Moulay El Hassan ikutane naye katika Fainali Juni 2.
    Huu unakuwa mwaka mzuri kwa Serengeti Boys kwa Tanzania katika ushiriki wake wa michuano ya U17 ya wavulana, ikiweka rekodi nyingine ya kwenda Fainali baada ya kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza sambamba na kufuzu Kombe la Dunia.  
    Mafanikio hayo yanakuja Tanzania ikishiriki kwa kwa mara ya tatu AFCON U17 baada ya mwaka 2017 nchini Gabon na 2019 nyumbani, Tanzania ambako mara zote walitolewa katika hatua ya makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANZANIA YATINGA FAINALI AFCOM U17, YAITOA MISRI KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top