TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Mashujaa Queens jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba Queens inafikisha pointi 56 na kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara ikiwa imebakiza mechi moja – kwani wapinzani, Yanga Princess na JKT Queens wote hawawezi kufikisha idadi hiyo ya pointi.
Hiyo inakuwa mara ya tano kwa Simba SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara na kuendelea kuwa timu hiyo iliyochukua mara nyingi zaidi taji hilo, ikifuatiwa na JKT Queens iliyobeba mataji hayo mara nne.
Timu nyingine iliyowahi kutwa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara ni Mlandizi Queens ambao walikuwa mabingwa wa kwanza msimu wa 2016 – 2017.
MABINGWA LIGI YA WANAWAKE
2025 – 2026: Simba Queens
2024 – 2025: JKT Queens
2023 – 2024: Simba Queens
2022 – 2023: JKT QUEENS
2021 – 2022: Simba Queens
2020 – 2021: Simba Queens
2019 – 2020: Simba Queens
2018 – 2019: JKT Queens
2017 – 2018: JKT Queens
2016 – 2017: Mlandizi Queens



.png)
0 comments:
Post a Comment