TIMU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, maarufu kama UEFA Champions League baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Arsenal ya England kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 120 usiku huu Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest nchini Hungary.
Haukuwa ushindi mwepesi kwa ‘Wana Paris’, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Ujerumani, Kai Lukas Havertz kuanza kuwafungia Washika Bunduki wa London dakika ya sita ya mchezo huo – kabla ya kiungo mwingine mshambuliaji, Mfaransa Masour Ousmane Dembélé mwenye asili ya Afrika kuwasawazishia kwa mkwaju wa penalti dakika ya 65.
Dembele anazaliwa na baba kutoka Mali na mama kutoka Waly Diantang, Kijiji kilichopo mkoa wa Gorgol, Kusini mwa Mauritania, jirani na Mto Senegal.
Waliofunga penalti za PSG ni mshambuliaji Mreno Gonçalo Matias Ramos, kiungo mshambuliaji Mfaransa Désiré Nonka-Maho Doué mwenye asili ya Ivory Coast na mabeki Mmorocco Achraf Hakimi Mouh na Mbrazil Lucas Lopes Beraldo, huku beki mwingine, Mreno Nuno Alexandre Tavares Mendes mwenye asili ya Cape Verde pekee akikosa.
Waliofunga penalti za Arsenal ni washambuliaji Msweden, Viktor Einar Gyökeres, Muingereza, Declan Rice na Mbrazil Gabriel Teodoro Martinelli Silva huku kiungo Muingereza, Eberechi ‘Ebere’ Oluchi Eze mwenye asili ya Nigeria na beki Mreno, Gabriel dos Santos Magalhaes wote wakikosa.
Hilo linakuwa taji la pili kihistoria la UEFA Champions League kwa Paris Saint-Germain – wakichukua mfululizo na mafanikio yote wakipata chini ya kocha Mspaniola, Luis Enrique Martínez García.



.png)
0 comments:
Post a Comment