• HABARI MPYA

    Wednesday, September 05, 2018

    YANGA SC KUMENYANA NA AFRICAN LYON JUMAPILI MECHI YA KIRAFIKI DAR BAADA YA KUFUTA SAFARI YA KIGOMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    VIGOGO wa soka Tanzania, Yanga SC watakuwa na mchezo wa kirafiki Jumapili dhidi ya African Lyon kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Yanga SC imeamua kumenyana na wapinzani wao hao wa Dar es Salaam baada ya kufuta mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Singida United iliyopangwa kufanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma leo.
    Baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuzuia timu kwenda Kigoma kwa sababu ya umbali, uongozi umefanikiwa kupata mechi ya karibu.

    Yanga SC inataka kuutumia mchezo huu kuiandaa timu yake kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu, dhamira yake kubwa ikiwa ni kutwaa ubingwa wa. 
    Sasa kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi Uwanja wa Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Polisi, Kurasini mjini Dar es Salaam.
    Mechi za Yanga za Ligi, pamoja na za Azam FC na Simba zimesimamishwa kupisha maandalizi ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania na Uganda Jumamosi mjini Kampala.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC KUMENYANA NA AFRICAN LYON JUMAPILI MECHI YA KIRAFIKI DAR BAADA YA KUFUTA SAFARI YA KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top