• HABARI MPYA

  Saturday, September 08, 2018

  WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR ‘WALILIA’ FEDHA ZAO ZA USHINDI WA MICHUANO YA KOMBE LA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WACHEZAJI wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro wamelalamika kutopatiwa fedha zao za ushindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kama walivyoahidiwa na uongozi wao.
  Wakizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, wachezaji hao wamesema kwamba uongozi wa Mtibwa Sugar uliwaahidi wachezaji kuwapa fedha zote, Sh. Milioni 50, ambazo hutolewa na wadhamini Azam TV.
  “Sisi tunashanga hadi leo viongozi hawajatupa hizi fedha na si kawaida yao, sisi kila tunachoahidiwa huwa tunapewa mapema tu, hatujui hapa imekuwaje, lakini wanatakiwa watupe haki yetu,”amesema mmoja wa wachezaji wa Mtibwa ambaye hakutaka kutajwa jina.


  Mtibwa Sugar wakisherehekea na Komba lao la TFF baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Singida United Juni 2, mwaka huu 

  Viongozi wa Mtibwa Sugar hawakupatikana leo walipotafutwa kuzungumzia malalamiko ya wachezaji wao, lakini habari zaidi zinasem kwamba na wao bado wanasotea fedha hizo kutoka TFF.
  Bin Zubeiry Sports – Online inafahamu, wadhamini wa michuano hiyo kampuni ya Azam TV wamekabidhi fedha zote kwa TFF. 
  Viongozi wa TFF nao hawakupatikana kuzungumzia habari hizo kwa sababu wameongozana na timu ya taifa kwenye mchezo dhidi ya Uganda leo.
  Inafahamika TFF inakabiliwa na hali ngumu kifedha, hususan baada ya kupoteza udhamini wa kampuni ya Vodacom kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Juni 2, mwaka huu Mtibwa Sugar ilitwaa Komba la TFF baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR ‘WALILIA’ FEDHA ZAO ZA USHINDI WA MICHUANO YA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top