• HABARI MPYA

  Wednesday, September 12, 2018

  SHERMAN WA YANGA AIFUNGIA LIBERIA IKICHAPWA 2-1 NA NIGERIA MECHI YA KUSTAAFISHA JEZI YA WEAH MONROVIA

  Na Mwandishi Wetu, MONROVIA
  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman jana aliifungia timu yake ya taifa, Liberia ikichapwa 2-1 na Nigeria katika mechi ya kuistaafisha jezi ya gwiji na Rais wa nchi hiyo, George Weah.
  Rais wa Liberia, George Weah jana aliichezea mechi ya kirafiki nchi yake akiwa ana umri wa miaka 51 ikifungwa 2-1 na Nigeria mjini Monrovia.
  Weah, mwanasoka wa kwanza wa Afrika kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia wa FIFA, alicheza kwa dakika 79 iliyoandaliwa maalum kuistaafisha jezi namba  14 iliyokuwa inatumiwa na gwiji huyo enzi zake.
  Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman akiifungia Liberia kwa penalti jana

  Rais wa Liberia, George Weah jana aliichezea Liberia akiwa ana umri wa miaka 51 

  Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan, aliyechaguliwa kuwa Rais wa Liberia Januari mwaka huu, alipewa heshia maalum wakati anatolewa uwanjani.
  Nigeria iliteremsha kikosi chake kamili kilichohusisha nyota wake kama Wilfred Ndidi wa Leicester City na kiungo mwenzake, Peter Etebo wa Stoke City zote za England.  Ndidi na mchezaji mwenzake, Kelechi Iheanacho waliingia kipindi cha pili.
  Mabao ya Super Eagles yalifungwa na Henry Onyekuru anayecheza kwa mkopo Galatasaray kutoka Everton na Simeon Nwankwo akimalizia kona ya Etebo, wakati la Liberia lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman kwa penalti.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHERMAN WA YANGA AIFUNGIA LIBERIA IKICHAPWA 2-1 NA NIGERIA MECHI YA KUSTAAFISHA JEZI YA WEAH MONROVIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top