• HABARI MPYA

  Monday, September 10, 2018

  SASA UKIAGIZA TIMU YA NJE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NCHINI BILA RUHUSA YA TFF HAIFANYIKI

  Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kupitia Mkugurugenzi wake wa Mashindano, Salum Madadi limezuia timu za nje ya nchi kuja kucheza mechi ya kirafiki au kushiriki mashindano mabalimbali nchini  bila kibali cha shirikisho hilo.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Madadi amesema kwamba taratibu zilizowekwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) zinazosimamiwa na vyama vya soka vya nchi wanachama wake zinapaswa kueshimiwa.
  Madadi, kocha wa zamani wa klabu mbalimbali na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema agizo hilo linawahusu wanachama wote wa shirikisho hilo ambao ni vyama vya soka vya mkoa, klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la kwanza, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Tatu na wengineo.

  Mkurugenzi huyo amesema wamelazimika kutoa onyo hilo baada ya matukio ya hivi karibuni ya kualikwa kwa timu za Kenya kuja kucheza mechi za kirafiki katika mikoa ya Dar es salaam na Mara bila kufuata taratibu za TFF kwa mujibu wa kanuni ya 15 ya Ligi Kuu kifungu cha kwanza, cha tatu hadi cha nane.
  Mkurugenzi huyo amesema pamoja na matakwa ya kanuni za Ligi Kuu kwa mechi za kirafiki wakati ligi inaendelea ni lazima taratibu za FIFA zifuatwe ili mchezo wa kirafiki wa kimataifa uwe halali.
  “Taratibu hizo ni kama ifuatavyo, ni lazima idhini itolewa na chama au Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi husika kwa klabu husika inayotaka kwenda nje ya nchi yake kucheza mechi za kirafiki, alisema Madadi.
  Madadi alitolea mfano mchezo wa kirafiki Simba SC na AFC Leopards ya Kenya uliofanyika Jumamosi Uwanja wa Taifa mjini Dar es Saalam kwamba ilihitajika barua kutoka Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) kuja TFF likionyesha klabu hiyo kuruhusiwa kuja nchini.
  “Shirikisho la Mpira la nchi mwenyeji ni lazima liombe kibali kutoka FIFA, kuna fomu maalamu lazima tuzijaze ili mchezo huo uwe halali na kwenye fomu hiyo ni lazima tuainishe mahali mpira utakapochezewa, tarehe, waamuzi na mamlaka iliyowateua waamuzi hao na baada ya kutimiza hizo hatua muaandaji wa mchezo huo lazima apate kibali kutoka TFF. Nimesisitiza utaratibu huu, maana ukikiukwa Shirikisho lazima lipate adhabu,” alisema Madadi.
  Pamoja na Leopards kufanikiwa kucheza na Simba na kufungwa 4-2, lakini mechi yake ya pili iliyokuwa ifanyike Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ilifutwa na TFF kwa sababu taratibu hizo hazikufuatwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SASA UKIAGIZA TIMU YA NJE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NCHINI BILA RUHUSA YA TFF HAIFANYIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top