• HABARI MPYA

    Thursday, September 13, 2018

    PEPE REINA NDIYE KIPA BORA WA KIHISTORIA ENGLAND

    KIPA wa zamani wa Liverpool, Pepe Reina ameibuka kinara wa kudaka mechi nyingi za Ligi Kuu ya England kihistoria.
    Mspaniola huyo, ambaye kwa sasa anachezea AC Milan ya Italia, alicheza Anfield kati ya mwaka 2005 na 2013, akidaka jumla ya mechi 285 za Ligi Kuu wakati huo.
    FourFourTwo imehesabu mechi ambazo makipa walidaka kufungwa katika Ligi Kuu ya England tangu mwaka 1992, ikiwahusisha makipa waliodkaa kuanzia mechi 50 tu.
    Na ni Reina ambaye ameibuka kinara, akiwapiku walinda milango wengine hodari wakiwemo Edwin van der Sar na Petr Cech kwa asilimi yake 47.02 jumla ya kudaka bila kufungwa. 
    Kipa wa zamani wa Chelsea anayedakia Arsenal kwa sasa, Cech amechukua Medali ya Fedha kwa asilimi zake 45.68, wakati Mholanzi Van der Sar amekamata nafasi ya tatu kwa asilimia zake 42.17.
    Mwingine aliyeingia tano bora ni kipa gwiji wa Denmark, Peter Schmeichel (asilimia 41.29) na gwiji wa Arsenal, David Seaman (asilimia 40.70).
    Kipa wa Tottenham na Chelsea, Mtaliano, Carlo Cudicini alidaka mechi 64 bila kufungwa kati ya 161, inayomfanya apate asilimia 39.75.
    Tomasz Kuszczak, aliyewahi kudakia Manchester United, kwa mastaajabu ameingia 10 Bora kwa asilimi zake 39.68 wakati Manuel Almunia, aliyedaka mechi 109 jumla, amepata asilimia 39.45.
    Bobby Mimms ambaye pamoja na bahati mbaya ya kukosa Medali ya ushindi wa taji la Ligi Kuu ya England akiwa Blackburn baada ya klabu kumsajili Tim Flowers kama namba moja wao mpya mwaka 1993, lakini amepata asilimia 39.34, inayomfanya ashike nafasi ya tisa.
    David de Gea, kipa bora kabisa kwa sasa katika Ligi Kuu ya England, anakamata nafasi ya 10 kwa asilimia zake 39.00. Wengine walioingia kwenye 20 Bora ni pamoja na Joe Hart, Thibaut Courtois na Thomas Myhre.

    Pepe Reina ameibuka kinara wa kudaka mechi nyingi za Ligi Kuu ya England kihistoria 


    ORODHA YA MAKIPA 20 BORA LIGI KUU YA ENGLAND KWA KUDAKA MECHI NYINGI BILA KUFUNGWA 

    1) Pepe Reina – Mechi 285; kati ya hizo 134 hakufungwa; 47.02%
    2) Petr Cech – Mechi 440; kati ya hizo 201 hakufungwa; 45.68%
    3) Edwin van der Sar – Mechi 313; kati ya hizo 132; 42 hakufungwa.17%
    4) Peter Schmeichel – Mechi 310; kati ya hizo 128 hakufungwa; 41.29%
    5) David Seaman – Mechi 344; kati ya hizo 140 hakufungwa; 40.70%
    6) Carlo Cudicini – Mechi 161; kati ya hizo 64 hakufungwa; 39.75%
    7) Tomasz Kuszczak – Mechi 63; kati ya hizo 25 hakufungwa; 39.68%
    8) Manuel Almunia – Mechi 109; kati ya hizo 43 hakufungwa; 39.45%
    9) Bobby Mimms – Mechi 61; kati ya hizo 24 hakufungwa; 39.34%
    10) David De Gea – Mechi 241; kati ya hizo 94 hakufungwa; 39.00%  
    11) Jerzy Dudek – Mechi 127; kati ya hizo 49 hakufungwa; 38.58%
    12) Joe Hart – Mechi 325; kati ya hizo 124 hakufungwa; 38.15%
    13) Thibaut Courtois – Mechi 126; kati ya hizo 48 hakufungwa; 38.10%
    14) Ed De Goey – Mechi 123; kati ya hizo 46 hakufungwa; 37.40%
    15) Nigel Martyn – Mechi 372; kati ya hizo 137 hakufungwa; 36.83%
    16) Jens Lehmann – Mechi 148; kati ya hizo 54 hakufungwa; 36.49%
    17) Wojciech Szczesny – Mechi 132; kati ya hizo 48 hakufungwa; 36.36%
    18) Mark Bosnich – Mechi 206; kati ya hizo 74 hakufungwa; 35.92%
    19) Hugo Lloris – Mechi: 209; kati ya hizo 75 hakufungwa; 35.89%
    20) Thomas Myhre – Mechi: 93; kati ya hizo: 33 hakufungwa; 35.48%
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PEPE REINA NDIYE KIPA BORA WA KIHISTORIA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top