• HABARI MPYA

  Sunday, September 16, 2018

  KABWILI AONDOLEWA KAMBINI YANGA KWA KUCHELEWA KURIPOTI, APEWA ONYO ATARUDI KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA mdogo wa Yanga, Ramadhani Awam Kabwili jana aliondolewa kambini baada ya kuchelewa kuripoti – hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo wa leo dhidi ya Stand United.
  Yanga inawakaribisha Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni ya leo. 
  Na jana kocha Mwinyi Zahera kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alimrudisha nyumbani Kabwili baada ya kuchelewa kuripoti.
  Msemaji wa Yanga, Dismass Ten ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba hakuna tatizo zaidi kati ya Kabwili na klabu au kocha na Jumatatu atendelea na mazoezi ingawa amepewa onyo kali asiruide.

  Ramadhani Kabwili (kulia) akiwa na kocha wa Azam Akademi, Iddi Cheche 

  Ten amesema kwamba kwa Kabwili ni mara ya kwanza kabisa anachelewa kambini tangu amejiunga na timu Januari mwaka huu kufuatia kung’ara akiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
  Kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuanza leo dhidi ya Stand United ni; Klaus Kindoki, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Feisal Salum, Mrisho Ngassa, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Ibrahim Ajib na Deus Kaseke.
  Katika benchi wapo; Benno Kakolanyam, Jaffar Mohammed, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Thabani Kamusoko, Raphael Daudi, Yussuf Mhilu na Amissi Tambwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KABWILI AONDOLEWA KAMBINI YANGA KWA KUCHELEWA KURIPOTI, APEWA ONYO ATARUDI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top