Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano na Benki ya Posta nchini juu
ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa
zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa
wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Tovuti ya Yanga SC, imeandika kwamba Mkurugenzi Masoko wa Benki ya
Posta nchini Bw. Deo Kwiyukwa amesema
wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi na kuona njia hiyo
itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa kuandikisha wanachama
utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.
"Badala ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza
fomu za uanachama watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi
za Benki ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama"
alisema Deo.
Gharama za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=,
na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya
TPB yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa
huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Naye Makaumu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema
anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia
mfumo huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi
zaidi na taarifa zetu zitaweza kuwafikia
wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe
16.05.2014 kwenye hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro
Hotel) na mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama
kutoka kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
0 comments:
Post a Comment