BONDIA Floyd Mayweather ameendelea kuonyesha jeuri ya fedha, baada ya kuwapa vimwana wawili kazi ya kumuhesabia dola zake za Kimarekani 100,000 taslimu kitandani, huku akitumia moja ya saa zake za gharama chafu kuangalia muda nani atamaliza haraka kuhesabu.
Mayweather alishinda kwa pointi pambano dhidi ya Marcos Maidana mjini Las Vegas Jumamosi usiku na kuunganisha mataji ya uzito wa Welter, akifikisha mapambano 46 ya ndondi za kulipwa bila kupoteza hats moja.
Jeuri ya fedha: Mayweather akiwatazamia muda katika saa mabinti wakati wanahesabu dola 100,000 kitandani
Mmarekani huyo akiwa ameshika begi ndogo ya saa zake 18 za bei ghal, amepost akisema: '@thatjessilee na @badmedina wanacheza gemu, kuona mani atahesabu haraka cola 100,000. Hiki ndicho huwa wanachokifanya wanaboreka. #TheMoneyTeam #FollowBeautifulLadies'
Ni haki kusema cola 100,000 ni ndogo mno kwa bingwa wa dunia mara tano, ambaye ametajwa kuingiza dola Milioni 70 katika pambano la Maidana. Amelipwa dola Milioni 32 za pambano, lililofanyika MGM Grand, na pia inaelezwa amelipwa dola Milioni 38 za haki ya matangazo ya Televisheni.
Mabinti wawili waliopigwa picha, Jessi Lee na Doralie Medina, ni sehemu ya wapambe wa Mayweather maarufu kama The Money Team (TMT).
Wachezea fedha: Doralie Medina, maarufu kama badmedina katika Instagram ni mmoja wa vimwana wawili waliokuwa wakihesabu fedha za Mayweather kitandani
Utamu huo: Binti mwingine aliyekuwa akihesabu fedha za Mayweather ni Jessi Lee
Sare sare: Jessi Lee akiwa na bosi wa The Money Team
0 comments:
Post a Comment