// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SI UTAJIRI, SI UMASIKINI BALI SIMBA NA YANGA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SI UTAJIRI, SI UMASIKINI BALI SIMBA NA YANGA... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, May 11, 2014

    SI UTAJIRI, SI UMASIKINI BALI SIMBA NA YANGA...

    VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga wapo katika michakato ya uchaguzi baada ya tawala za sasa kumaliza muda wake.
    Wakati michakato hiyo ikiwa katika hatua za mwanzoni, kama ilivyo ada tayari makundi ya makada au ‘wachumia tumbo’ yameanza harakati nayo za kushawishi wanachama wenzao juu ya aina ya viongozi wa kuchagua.
    Pande zote mbili, Simba na Yanga wamesikika wanachama kutoka makundi ya wachumia tumbo wakisema hawataki viongozi wenye fedha.
    Hiyo ni kwa sababu viongozi wanaomaliza muda walionekana kama matajiri, lakini wakashindwa kuziletea mafanikio klabu hizo.

    Yanga SC walikuwa wana bilionea Yussuf Manji na Simba SC walikuwa wana mwanasiasa na mfanyabiashara Alhaj Ismail Aden Rage, lakini wote wanaondoka klabu zikiwa hazina cha kujivunia kutokana na kuwepo kwao madarakani.
    Labda Rage atatamba aliwafunga Yanga 5-0, lakini Manji hana cha kuwaambia wanachama wake siku anaachia rasmi madaraka.
    Kwa sababu hiyo, wanachama hao wanataka kuwashawishi wenzao, wachague viongozi wasio na fedha, wakiamini hao ndiyo wana maarifa ya kuendesha klabu.
    Wanaposema hivyo wanajenga na hoja nzuri za ushawishi kwamba miaka ya mwanzoni ya uwepo wa klabu hizo, hakukuwa na watu wenye fedha, lakini waliweza kujenga misingi imara katika klabu.
    Majengo yote ya klabu hizo yalikuja wakati ambao klabu hizo zinaongozwa na waswahili wa mjini wavaa kanzu na makubazi- lakini wavaa suti leo wameshindwa kuleta jipya.
    Ni kweli katika zama mpya za klabu hizo kongwe hakuna jipya lililofanyika- lakini pamoja na hayo lazima wanachama wa klabu hizo watazame walipojikwaa na si walipoangukia.
    Katika zama hizi za sayansi na teknolojia tunahitaji viongozi weledi, waadillifu ambao watakuwa na mipango ya kuzifanya klabu hizo zibadilike ili kuendana na wakati.
    Haitakuwa vyema kuanza kuleta sera za ubaguzi wa watu katika uchaguzi, kama yule masikini, au yule tajiri, bali mwanachama atambuliwe kwa kadi yake na baada ya hapo apimwe kwa weledi wake, uadilifu na hekima.
    Simba na Yanga zimepitia mikononi mwa viongozi ambao tunawaita masikini na pia hazikunufaika na chochote na hao tunaowaita matajiri na pia kwa bahati mbaya wametoka kapa.
    Tusiwatazame watu kwa hali zao, bali tuwapime kwa weledi wao, uadilifu na hekima- lazima mgombea uongozi wa Simba au Yanga awaambie kwanza wanachama wenzake ameyafanyia nini maisha yake, ili waamini anaweza kuleta mageuzi katika klabu. 
    Mtu ambaye ameshindwa kuyamudu maisha yake pekee kwa kuyafanya yawe bora, huyo hawezi kuifanyia lolote klabu.
    Lakini anaweza akawa ana maisha bora, ila si mweledi, si mwadilifu na hana hekima, basi huyo pia hafai kuongoza klabu. 
    Wanachama wa Simba na Yanga SC lazima wawe makini sana katika wakati huu na vyombo vya habari vinapaswa kutumia kipindi hiki kuwaelimisha.
    Vyombo vya habari visikubali kuwapa nafasi wapotoshaji kupotosha wanachama wa klabu hizo- bali vyenyewe viwe mstari wa mbele kuwaelimisha wanachama.
    Simba SC na Yanga zinahitaji viongozi weledi, wabunifu, waadilifu na wenye hekima ambao wakiingia madarakani watatengeneza mipango ya kuleta mabadiliko ndani ya klabu hizo.
    Hadi sasa, Simba na Yanga bado hazijatumia vyema fursa zilizojaaliwa kuwa na majengo katikati ya mji, kuwa na mamilioni ya wafuasi mambo ambayo yanafanya nembo zake ziwe za thamani ya juu.
    Jamani, jezi makorokoro mengine mengi yenye nembo za Simba na Yanga zinauzwa kwa wingi nchini kote, lakini huwezi kujua ni kiasi gani cha fedha kinaingia klabuni.
    Lakini kama Simba na Yanga zitapata viongozi wa maana watakwenda kusimamia hayo na mengine pia ili kuzijengea misingi imara klabu hizo.
    Simba na Yanga SC zikipata viongozi bora, zitaendelea kuwa klabu imara na bora Tanzania- lakini kama zitarudia makosa katika uchaguzi wa viongozi, basi zitazidi kuporomoka.
    Fedha, au umasikini kwa ujumla hali ya mtu si kigezo cha kuchagua kiongozi, bali mtu atazamwe kwa weledi wake, uadilifu, hekima na labda historia yake na klabu, kuepuka kuchukua watu ambao ni mamluki. Alamsiki. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SI UTAJIRI, SI UMASIKINI BALI SIMBA NA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top