| Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Mrundi Suleiman Ndikumana akikaribishwa katika klabu yake mpya, El Merreikh ya Sudan ambayo imenunua baada ya Mrisho Ngassa wa Simba SC kukataa nafasi hiyo. Merreikh ilikuwa tayari kumnunua Ngassa kwa dola za Kimarekani 150,000 (zaidi ya Sh Milioni 230) ambazo zingelipwa kwa klabu zake, Simba SC anakocheza kwa mkopo kutoka Azam FC. Yeye mwenyewe angelipwa dau la dola 100,000 (zaidi ya Sh Milioni 150) la kusaini na mshahara wa dola 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5). Lakini aliitema ofa huyo na anaendelea na mshahara wa Milioni 2, kwa mwezi Simba SC. Picha kwa hisani ya Ndikumana mwenyewe. |