• HABARI MPYA

    Tuesday, September 18, 2018

    ZAHERA MOTO YANGA, AWASIMAMISHA MNGWALI, MAKAPU NA BUSWITA KWA UTOVU WA NIDHAMU

    Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mwinyi Zahera, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewasimamisha wachezaji watatu wa klabu hiyo, beki Mwinyi Hajji Mngwali na viungo Said Juma Makapu na Pius Buswita kwa utovu wa nidhamu.
    Wachezaji hao walimkera kocha Zahera kwa kutozingatia muda juzi, wakati timu inajiandaa kwenda kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United.
    Na Zahera ambaye pia kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DRC akawaondoa kambini na kuwaambia waendelee kutumikia adhabu hadi baada ya mechi ya kesho dhidi ya Coastal Union.
    Yanga SC inatarajiwa kuwaalika mabingwa wenzao wa zamani wa Ligi Kuu, Coastal Union katika mchezo uliopangwa kuanza Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa.

    Pius Buswita amesimamishwa Yanga SC kwa utovu wa nidhamu 

    Habari njema kuelekea mchezo huo ni kwamba beki Juma Abdul Jaffar Mnyamani aliyekosekana kwenye mechi na Stand United, Yanga ikishinda 4-3 amerejea.
    Abdul amefanya mazoezi jana na leo kuelekea mchezo wa kesho unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na historia ya kila Yanga inapokutana na Coastal.  Kungo Juma Mahadhi ndiye pekee hayuko fiti, lakini ameanza mazoezi mepesi ya peke yake.
    Kipa Ramadhani Kabwili aliyeondolewa kambini Jumamosi kwa utovu wa nidhamu pia, adhabu yake imeisha na jana na leo amefanya mazoezi.
    Kipa Benno Kakolanya aliyekuwa majeruhi amepona na jana na leo amefanya mazoezi pamoja na mlinda mlango, Klaus Kindoki raia wa DRC aliyekuwa langoni juzi, Yanga ikifungwa mabao matatu na Alex Kitenga, japo ilishinda 4-3. 
    Yanga inahitaji kushinda mechi ya tatu mfululizo nyumbani, baada ya awali kushinda dhidi ya Mtibwa Sugar 2-1 na juzi 4-2 na Stand United.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAHERA MOTO YANGA, AWASIMAMISHA MNGWALI, MAKAPU NA BUSWITA KWA UTOVU WA NIDHAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top