• HABARI MPYA

  Tuesday, September 18, 2018

  SIMBA SC YAWASILI MWANZA LAKINI MASUD JUMA KWA MARA NYINGINE AMEBAKI DAR…SAFARI IMEIVA?

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba SC kimewasili mjini Mwanza asubuhi ya leo kwa ndege tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzani Bara dhidi ya wenyeji, Mbao FC Alhamisi Uwanja wa CCM Kirumba.
  Lakini kwa mara nyingine, kocha Mrundi, Masoud Juma amebaki mjini Dar es Salaam bila sababu zenye kueleweka haswa.
  Masoud alibaki Dar es Salaam wakati Simba SC ikilazimishwa sare ya 0-0 na Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara Jumamosi na uongozi ukasema ilikuwa kwa sababu maalum.
  Lakini tayari kuna taarifa kwamba Masoud ametofautiana na uongozi wa klabu na ni kama amewekwa kando kwa manufaa ya timu huku taratibu za kuachana naye moja kwa moja zikiendelea.

  Juma aliwasili nchini Oktoba 19, mwaka mwaka jana akitokea Rwanda alipokuwa anafundisha timu ya Rayon Sport, kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha Msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja aliyeng’atuka.
  Alianza kazi chini ya Mcameroon, Joseph Omog lakini akafukuzwa, akaletewa Mfaransa, Pierre Lechantre aliyemalizia msimu na timu ikatwaa ubingwa kabla ya kufukuzwa – na Mbelgiji, Patrick J Aussems anakuwa kocha wa tatu mkuu wa Mrundi huyo.
  Lakini wakati Lechantre anaondoka alimtupia lawama Juma akidai alimsaliti na inaelezwa alitafuta nafasi ya kuzungumza na Aussems kumueleza juu ya kocha huyo wa Burundi. 
  Bado uongozi wa Simba SC unasubiriwa kutoa hatma ya Masoud ambaye tangu Oktoba mwaka jana amekuwa Kaimu Kocha Mkuu mara mbili na timu ikaendelea kufanya vizuri. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWASILI MWANZA LAKINI MASUD JUMA KWA MARA NYINGINE AMEBAKI DAR…SAFARI IMEIVA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top