• HABARI MPYA

  Tuesday, September 18, 2018

  MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO DIFAA HASSAN EL JADIDI IKISHINDA 2-1

  Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN 
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefunga bao la pili timu yake, Difaa Hassan El Jadidi ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Khouribga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco ijulikanayo kama Botola Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan. 
  Msuva aliyekuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilicholazimisha sare ya 0-0 na wenyeji Uganda Uwanja wa Mandela mjini Kampala Septemba 8, jana alifunga bao lake dakika ya 82 kufuatia Karim El Hachim kufunga la kwanza dakika ya 73.
  Khouribga wakapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Youssef Ogaddi dakika ya 89 akitumia makosa ya walinzi wa Difaa Hassan El Jadidi kujisahau.
  Simon Msuva (kulia) akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Difaa Hassan El Jadidi
  Simon Msuva (kulia) akimiliki mpira mbele ya beki wa Khouribga

  Simon Msuva mbele kulia katika kikosincha Difaa Hassan El Jadidi kilichoanza jana

  Ushindi wa jana unaifanya DHJ kufikisha pointi sita baada ya mechi mbili za mwanzo ikishinda zote na kuwa kileleni mwa Botola, ikifuatiwa na FUS Rabat yenye pointi nne sawa na Rapide Oued Zem.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA AENDELEZA MOTO WA MABAO MOROCCO DIFAA HASSAN EL JADIDI IKISHINDA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top