• HABARI MPYA

  Monday, May 07, 2018

  YANGA YAANZA VIBAYA HATUA YA MAKUNDI AFRIKA…YABOMOLEWA 4-0 ALGIERS HADI HURUMA

  Na Mwandishi Wetu, ALGIERS
  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC usiku huu wameanza vibaya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 4-0 na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Daniel Nii Ayi Laryea aliyesaidiwa na David Laryea wote wa Ghana na Abel Baba wa Nigeria hadi mapumziko, USMA walikuwa walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
  Mabao hayo yalifungwa na Oussama Darfalou dakika ya nne kwa kichwa akimalizia krosi ya Mohamed Rabie Meftah na Farouk Chafai dakika ya 33 akimalizia kazi nzuri ya Faouzi Yaya.


  Wachezaji wa USMA wakimpongeza kipa wao, Mohamed Amine Zemmamouche baada ya kufunga bao la nne dakika ya mwisho

  Kipindi cha pili Yanga ilikianza kidogo kwa kujaribu kushambulia, lakini taratibu ikarejea kwenye mchezo wake wa kujihami zaidi.

  Na haikuwa ajabu iliporuhusu mabao mawili zaidi, la tatu likifungwa na Abderrahmane Meziane dakika ya 54 akimalizia kazi nzuri ya Ayoub Abdellaoui na la nne lilifungwa kwa penalti na kipa Mohamed Amine Zemmamouche dakika ya 90 na ushei baada ya beki wa Yanga SC, Andrew Vincent Chikupe kumchezea rafu Darfalou.
  Wachezaji wawili wa Yanga, Kessy na Mahadhi walionyeshwa kadi za njano leo sawa na Darfalou wa U.S.M. ambaye leo alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya timu ya mjini Dar es Salaam nchini Tanzania. 
  Mechi nyingine ya leo ya Kundi D; wenyeji Rayon Sport wamelazimishwa sare ya kufungana bao1-1 na  Gor Mahia Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali.
  Gor Mahia FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake mkongwe, Meddie Kagere dakika ya 10, kabla ya Eric Rutanga kuisawazishia Rayon Sport dakika ya 24.
  Yanga itateremka tena uwanjani Mei 16 kumenyana na Rayon Sport na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
  Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
  Kikosi cha USM Alger kilikuwa;  M. Zemmamouche, M. Meftah, F. Chafai, M. Benyahia, A. Abdellaoui/M. Benmoussa dk59, R. Bouderbal, M. Benkhemassa, A. Benguit/H. Koudri dk80, F. Yaya/A. Sayoud dk73, A. Meziane na O. Darfalou.
  Yanga SC; Youthe Rostand, Gardiel Michael, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Geoffrey Mwashiuya, Said Juma ‘Makapu’/Pato Ngonyani dk83, Juma Mahadhi, Yussuf Mhilu/Yohanna Nkomola dk78, Raphael Daudi/Juma Abdul dk62 na Pius Buswita.

  MATOKEO KAMILI MECHI ZA 

  UFUNGUZI HATUA YA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA 


  ASEC Mimosas1 - 0Aduana StarsView eventsMore info

  RSB Berkane1 - 0Al Hilal OmdurmanView eventsMore info

  Enyimba2 - 0DjolibaView eventsMore info

  Rayon Sports1 - 1Gor MahiaView eventsMore info

  Raja Casablanca0 - 0Vita ClubView eventsMore info

  Al Masry2 - 0SongoView eventsMore info

  WAC1 - 0CARA BrazzavilleView eventsMore info

  USM Alger4 - 0Yanga SC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA VIBAYA HATUA YA MAKUNDI AFRIKA…YABOMOLEWA 4-0 ALGIERS HADI HURUMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top