• HABARI MPYA

  Sunday, May 06, 2018

  YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA

  Na Mwandishi Wetu, ALGIERS
  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC leo wanatupa karata yao ya kwanza katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika watakapomenyana na wenyeji, U.S.M. Alger katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algiers kuanzia Saa 4:00 usiku.
  Yanga SC jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho Uwanja wa Julai 5, 1962 na wachezaji wake walionekana wachangamfu pamoja na hali ya hewa ya baridi kali mjini Algiers.
  Kocha Mkongo, Mwinyi Zahera anayesaidiwa na Mzambia, Noel Mwandila na wazawa Nsajigwa Shadrack na juma Pondamali kocha wa makipa walionekana wenye kujiamini kuelekea mchezo huo.
  Wachezaji watano nyota wa Yanga SC, mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, kiungo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na washambuliaji Ibrahim Ajib na Mzambia Obrey Chifrwa hawajasafiri na timu kwa sababu mbalimbali.
  Pamoja na Yanga na U.S.M. Alger, timu nyingine zilizpo Kundi D ni Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya ambazo zitamenyana zenyewe katika ufunguzi wa hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
  Baada ya mechi ya kwanza ugenini Jumapili, Yanga itamenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
  Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
  Kila la heri Yanga SC. Mungu ibariki Yanga DC, Mungu ibariki Tanzania. Amin. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAANZA KAZI AFRIKA LEO…WANAKIPIGA NA U.S.M. ALGER SAA 4:00 USIKU ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top