// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YAYA TOURE AFUNGUKA; "YOTE ALIYOSEMA WAKALA WANGU NI KWELI, NITAAMUA MUSTAKABALI WANGU BAADA YA KOMBE LA DUNIA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YAYA TOURE AFUNGUKA; "YOTE ALIYOSEMA WAKALA WANGU NI KWELI, NITAAMUA MUSTAKABALI WANGU BAADA YA KOMBE LA DUNIA" - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 20, 2014

    YAYA TOURE AFUNGUKA; "YOTE ALIYOSEMA WAKALA WANGU NI KWELI, NITAAMUA MUSTAKABALI WANGU BAADA YA KOMBE LA DUNIA"

    MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure ameibuka kumsapoti wakala wake, Dimitri Seluk aliyeishambulia Manchester City kwa kutojali kuhusu birthday ya kiungo huyo.
    Yaya amesema yote aliyoyasema Seluk ni ukweli mtupu na yeye ataamua mustakabali wake baada ya Fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao.
    Seluk ameelezea shaka ya mchezaji huyo wa Ivory Coast kubaki Etihad kwa kusema kiungo huyo tegemeo haifurahii na klabu hiyo.
    Na Toure ametweet: "Wakala wangu alikuwa anajaribu kuelezea ukweli kwa niaba yangu, utani pembeni. Inasemekana muhimu kwangu ni kutoa taarifa.. Nitafanya hivyo. Kila kitu alichosema Dimitry ni ukweli. Amenizungumzia. Nitatoa mahojiano ya kufafanua baada ya Kombe la Dunia,".
    Amekasirishwa: Yaya Toure amekasirishwa na kitendo cha Manchester kutojali kuhusu sherehe yake ya kuzaliwa

    Kiungo huyo wa Ivory Coast, ambaye amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake unaomfanya alipwe Pauni 220,000 kwa wiki, imeelezwa amechukiwa na kitendo cha kutotumiwa salamu za kufurahia miaka 31 ya kuzaliwa kwake. 
    Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema: "Kuna uwezekano mkubwa Yaya akaondoka majira haya ya joto. Amechukizwa. Kilichotokea katika birthday take kinamaanisha klabu haimjali. Imethibitika,"amesema.
    "Wanaweza kusema vyovyote watakavyo, Oh tunampenda lakini tulisahau. Kusahau? Kuhusu Yaya? Mchezaji ambaye amekufanya umeshinda mataji mawili ya Ligi Kuu? Kijana ambaye amekusaidia kushinda Kombe la FA na Kombe la Ligi?
    "Katika timu ya kawaida, wachezaji wenzake na klabu angalau wangempa salami za kumtakia heri. Lakini wakati umeshinda taji na siku mbili baadaye una pati kubwa kusherehekea taji na hakuna mtu aliyekwenda kumtakia happy birthday Yaya, nini zaidi unachotaka? 
    "Ikiwa mchezaji kama Yaya anakwenda Liverpool nawanashinda ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 24, Yaya atakuwa mzuri Liverpool,"alisema Seluk.
    Amemtolea mfano beki wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Roberto Carlos alipewa gari aina ya Bugatti Veyron wakati wa birthday yake na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE AFUNGUKA; "YOTE ALIYOSEMA WAKALA WANGU NI KWELI, NITAAMUA MUSTAKABALI WANGU BAADA YA KOMBE LA DUNIA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top