MWISHONI mwa wiki, timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ilianza rasmi zama mpya chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika 2005 nchini Morocco.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Joseph Odartei Lamptey aliyesaidiwa na Malid Alidu Salifu na David Laryea wote wa Ghana, hadi mapumziko tayari Taifa Stars walikuwa wamekwishapata bao hilo.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa mabingwa Bara, Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ dakika ya 13 akiunganisha kwa guu la kushoto krosi maridadi ya mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Ulimwengu.
Kwa matokeo hayo, Stars inaelekea kwenye kibaruwa kigumu katika mchezo wa marudiano mjini Harare Juni 1, ambako itatakiwa kulazimisha sare au kufungwa kwa tofauti ya bao moja nayo ikifunga ili kusonga mbele- kwa mfano 2-1, 3-2 au 4-3.
Pamoja na ushindi huo mwembamba, Stars haikucheza soka ya kuvutia sana na ilionekana wazi Nooij bado hajawaunganisha wachezaji kucheza kwa uelewano mzuri katika mfumo wa 4-4-3 alioutumia Jumapili.
Zimbabwe walitawala sehemu ya kiungo na Stars ilimtumia Thomas Ulimwengu zaidi kushambulia upande wa kulia ambaye alifanikiwa kutoa krosi ya bao.
Samatta na John Bocco waliocheza pamoja katikati ilionekana wanahitaji muda zaidi wa kucheza pamoja ili kuzoeana na baadaye waje kuwa pacha tishio.
Mrisho Ngassa kama kawaida alifanya vizuri, lakini alishindwa kushambulia sana kwa sababu alilazimika kumsaidia zaidi Mwinyi Kazimoto katikati ya Uwanja.
Beki wa kulia Shomary Kapombe alijitahjidi mno kusaidia mashambulizi, lakini mipira ilipomgeukia alikuwa anapitika kwa urahisi.
Beki wa kushoto, Osacr Joshua alizuia vizuri, lakini hakuweza kupanda kusaidia mashambulizi- wakati mabeki wa kati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kevin Yondan walijitahidi, lakini walipitika na kuliweka lango la Stars katika misukosuko mara kadhaa.
Kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliokoa michomo kadhaa lakini miwili ilimpita na kutolewa na mabeki wake ikiwa inaelekea kutinga nyavuni.
Zimbabwe waliokuwa wanacheza kwa kasi na nguvu wameonyesha ni timu hatari na wanaweza kuwa hatari zaidi watakapokuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao.
Nooij aliidhoofisha timu kipindi cha pili kwa mabadiliko aliyoyafanya akiwatoa kwa nyakati tofauti Frank Domayo, Ngassa na Bocco na kuwaingiza Amri Kiemba, Khamis Mcha ‘Vialli’ na Haroun Chanongo.
Thomas Ulimwengu ndiye aliyestahili kupumzishwa kipindi cha pili baada ya kazi kubwa aliyoifanya kipindi cha kwanza, kiasi cha kuonekana dhahiri alichoka.
Na Simon Msuva ndiye aliyestahili kumpokea, kwani winga huyo wa Yanga ana kasi na anateleza vizuri pembezoni mwa Uwanja.
Baada ya kupumzishwa shujaa wa mechi, Bocco, Amri Kiemba angeenda kuongeza idadi ya viungo ili kuiondoa safu hiyo katika utawala wa wageni.
Maana yake Haroun Chanongo na Mcha wasingeshiriki mchezo huo- na labda mabadiliko yangekuwa hivyo Stars ingeweza kuondoka na ushindi mnene kidogo.
Stars inaweza kuwapata mapema washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu katika mchezo wa marudiano, kwa sababu wikiendi ijayo klabu yao haitakuwa na mechi.
Wachezaji hao wikiendi hii watakuwa wakiitumikia klabu yao katika Ligi ya Mabingwa Afrika nyumbani mjini Lubumbashi dhidi ya mahasimu, AS Vita ya Kinshasa, DRC na katikati ya wiki ijayo wanaweza kujiunga na Stars.
Ikumbukwe mchezo wa Jumapili ulikuwa wa pili kwa kocha Nooij tangu arithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen baada ya awali kutoa sare ya bila kufungana na Malawi mjini Mbeya.
Bahati mbaya Nooij amekuja Tanzania wakati ambao ligi imesimama na hajapata fursa ya kuteua wachezaji kwa utashi wake- bali mapendekezo anayopewa.
Wazi Nooij bado hajawafahamu vizuri wachezaji na kwa sasa anachofanya ni kutumia uzoefu wake tu kujaribu kuiongoza timu hiyo.
Kwa matokeo yoyote yale baada ya mchezo wa marudiano, vyema ieleweke mapema- kocha huyo anahitaji muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri.
Aliiandaa timu mazoezini, akawaingiza wachezaji uwanjani wakacheza walivyocheza na kama mapungufu ameyaona, ubora wa wapinzani ameuona na bila shaka sasa angalau kuelekea mchezo wa marudiano atakuwa amepata mwanga fulani.
Alikuwa akijibu maswali kwa kujiamini katika Mkutano na Waandishi wa Habari na hakutaka kuongea sana juu ya timu yake, zaidi ya kusema atakwenda kucheza mpira Harare.
Pamoja na yote, anakwenda kucheza mchezo mgumu ambao kwa matokeo yoyote, hata mabaya- atastahili kupewa muda zaidi.
Tuiombee heri timu yetu ya taifa, iweze kuvuka mtihani huo mgumu na baada ya hapo, Nooij ajipange upya ili kuweza kuwa na timu nzuri ya ushindani. Mungu ibariki Tanzania, ibariki Taifa Stars. Amin.

0 comments:
Post a Comment