• HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    WALIO KATIKA RADA ZA WENGER ARSENAL YA KUTISHA MSIMU UJAO...NA WA KUTEMWA PIA HAWA HAPA

    MASHABIKI wa Arsenal watakuwa wanatumai ushindi wa Kombe la FA wa timu yao katika fainali dhidi ya Hull City Jumamosi ni mwanzo wa mataji mengi mengine klabuni kwao.
    Kocha wa Gunners, Arsene Wenger atakuwa anafahamu kikosi chake kinahitaji kuongezewa nguvu ya kiushindani kwa ajili ya msimu ujao.
    Kwa mtazamo huo, BIN ZUBEIRY inakuletea makala iliyoandikwa na mchambuzi wa Sportsmail, Sami Mokbel juu ya tathmini ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa na kutemwa Emirates.  
    Muhimu kusajiliwa;
    Victor Valdes (Kipa, huru) - Kipa huyo atakuwa huru wakati wa dirisha la usajili. Atahitaji mshahara mkubwa na Arsenal ipo vizuri kiuchumi hivi sasa.

    Usalama: Mustakabali wa Petr Cech katika klabu ya Chelsea utakuwa shakani iwapo kocha Jose Mourinho ataamua kumrejesha kipa Thibaut Courtois

    Petr Cech (Kipa, Chelsea) - Wenger anamkubali sana kipa huyo. Klabu itakuwa inafuatilia sakata linaloendelea hivi sasa, iwapo Chelsea itamrejesha Thibault Courtois anayedaka kwa mkopo Atletico Madrid, basi yeye anweza kuondoka. Courtois ametoa sharti la kurejea kama kipa wa kwanza.
    Serge Aurier (Beki, Toulouse) - Amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na was aka vipaji wa klabu na ameonyesha ni beki mzuri, kiasi kwamba ameingia kwenye mipango ya Arsenal.
    Micah Richards (Beki, Manchester City) - Anaweza kupatikana kwa day la Pauni Milioni 5. Akiwa ni shabiki wa Arsenal pia, anaweza kuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo akisajiliwa.
    Versatile: Micah Richards would cost the Gunners around £5million and he's an Arsenal fan
    Micah Richards anaweza kuigharimu The Gunners kiasi cha Pauni Milioni 5 tu ni shabiki wa Arsenal

    Callum Chambers (Beki, Southampton) - Amewavutia wasaka vipaji katika msimu wake wa kwanza. Anaweza kusajiliwa.
    Lars Bender (Kiungo, Bayer Leverkusen) - Wenger alijaribu kumsajili msimu uliopita. Dau lake linafikiriwa kuwa Pauni Milioni 20 na ni mchezaji wa aina ya wachezaji wa Arsenal.
    Morgan Schneiderlin (Kiungo, Southampton) - Hana umaarufu sana, lakini anapendwa mno na baadhi ya watt wa bench la Ufundi la The Gunners.
    Ilkay Gundogan (kiungo, Dortmund) - Kiungo anayemnyima usingizo Wenger, lakini hofu ya klabu ni kwamba hawezi kupatikana.
    Loic Remy (Mshambuliaji, QPR) - Amekuwa akihusishwa na kuhamia The Gunners, je hatimaye mwaka huu Arsene Wenger atamnyakua?
    Jackson Martinez (Mshambuliaji, Porto) - Rekodi nzuri ya kuvutia ya mabao Ureno. Baada ya klabu kumkosa Januari, bila shaka sasa itajaribu tena na thamani yake ni Pauni Milioni 34. 
    Pedigree: Real Madrid striker Karim Benzema would surely boost Arsenal's Premier League title hopes
    Matawi ya juu: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema hakika ataongeza nguvu kwenye kikosi cha Arsenal katika kampeni za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu

    Mario Mandzukic (Mshambuliaji, Bayern Munich) - Anaweza kuondoka Bayern Munich dirisha hili la usajili wakati Robert Lewandowski atakapowasili. Wazi Arsenal inamtaka.
    Karim Benzema (Mshambuliaji, Real Madrid) - Wenger amerudia tena na tena kujaribu bila mafanikio kumsajili Mfaransa mwenzake huyo. Sasa yuko tayari kujaribu tena.

    KIKOSI KINACHOFAA KUWA CHA KWANZA ARSENAL MSIMU WA 2014/15 XI

    Szczesny; Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Bender, Ramsey, Wilshere; Ozil, Cazorla; Benzema
    Gunner? Both Arsenal and Chelsea are rumoured to be in for the signing of Mario Mandzukic
    Atashika mtutu? Klabu zone  Arsenal na Chelsea zimeripoitiwa kuwania sainai ya Mario Mandzukic

    Wanaoweza kuondoka
    Lukasz Fabianski - Shujaa huyo wa ubingwa wa Kombe la FA ataondoka mkataba wake utakapomalizika mwezi ujao. Anatakiwa na Schalke.
    Emiliano Viviano - Muda wake wa kucheza kwa mkopo wa muds mrefu kutoka Palermo umemalizika na ataondoka Emirates.
    Bacary Sagna - Klabu imeshindwa kufikia makubaliano naye juu ya Mkataba mpya na anaweza kuhamia klanbu za Manchester. Litakuwa pigo kubwa.
    Off: Bacary Sagna (right) is yet to sign a new contract with the club and looks certain to leave
    Anaondoka: Bacary Sagna (kulia) bado hajasaini Mkataba mpya na inaonekana kama anataka kuondoka 

    Nacho Monreal - Alisajiliwa kama mbadala wa Kieran Gibbs katika beki ya kushoto, lakini hajaweza kuanya kazi ya kuvutia.
    Thomas Vermaelen - Nahodha huyo wa The Gunners alikuwa katika wakati mgumu msimu huu na anaweza kuomba kuondoka. Anaweza kutua Napoli.
    Kim Kallstrom - Atarejea Spartak Moscow baada ya kumaliza muds wake wa kucheza kwa mkopo.
    Mikel Arteta - Ulikuwa ni usajili wa maana  lakini shaka zimeanza akiwa amebaki miezi 12 katika Mkataba wake.
    Nicklas Bendtner - Mshambuliaji huyo anamaliza Mkataba wake mwezi ujao na uwezekano wa kubaki ni haba.
    Lukas Podolski - Amekuwa chachu ya mafanikio ya timu siku za karibuni, lakini alikoa mechi kibao za mwanzoni mwa msimu. Inter Milan inamfuatilia.
    Olivier Giroud - Anaweza kujikuta anaondoka katika kikosi cha kwanza baada ya usajili wa nyota wapya msimu ujao. Je, atakuwa na furaha kuanzia benchi? 
    Second best? Olivier Giroud has been Arsenal's star man but could get pushed down the pecking order
    Chaguo la pili bora? Olivier Giroud amekuwa nyota na tegemeo la Arsenal msimu huu, lakini anaweza kushuka baada ya kusajiliwa nyota wapya msimu ujao
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WALIO KATIKA RADA ZA WENGER ARSENAL YA KUTISHA MSIMU UJAO...NA WA KUTEMWA PIA HAWA HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top