Na Nagma Khalid, Dar es Salaam
‘KOMREDI’ Michael Riachard Wambura ameanza kula matunda ya utawala wa Jamal Emil Malinzi, rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupitishwa kugombea Urais wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam.
Wambura ambaye wakati wote wa utawala wa Leodegar Chillah Tenga amekuwa akizuiwa kugombea kila sehemu anayotia mguu, leo amepitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kuendelea kuwania Urais wa klabu hiyo.
Wagombea wote 41 waliochukua fomu na kurudisha wamepitishwa baada ya kupitiwa kwa fomu hizo na akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Damas Ndumbaro amesema baada ya kuwapitisha wagombea hao, zoezi linalofuata ni la pingamizi.
Amesema kila muweka pingamizi lazima awasilishe pingamizi lake kwa maandishi likiambatana na vithibitisho. “Pia pingamizi hili liwe na jina na anuani kamili la muweka pingamizi, namba ya simu pamoja na nakala ya kadi ya Simba, na nawe mwanachama hai na mwisho wa kutoa pingamizi ni Mei 22,”amesema.
Ndumbaro amesema kuwa pingamizi zitasikilizwa Mei 25 katika ukumbi wa Gymkhana, Dar es Salaam na wanaotakiwa kufika katika pingamizi hizo ni muweka na muwekewa pekee.
“Kamati itatoa maamuzi ya pingamizi Mei 27. Alisema baada ya hapo utafuata usaili wa kwa wale waliopita katika pingamizi ambao utafanyika Mei 29 katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay,”.
Ameongeza kuwa siku ya usaili wagombea wanatakiwa kufika na nakala halisi ya vyeti vyake, picha ndogo na risiti ambayo amelipia kadi yake ya uanachama kwa miaka mitatu na ambaye hatakuwa na risiti atakuwa amejitoa mwenyewe kwenye kinyang’anyiro.
‘KOMREDI’ Michael Riachard Wambura ameanza kula matunda ya utawala wa Jamal Emil Malinzi, rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupitishwa kugombea Urais wa klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam.
Wambura ambaye wakati wote wa utawala wa Leodegar Chillah Tenga amekuwa akizuiwa kugombea kila sehemu anayotia mguu, leo amepitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC kuendelea kuwania Urais wa klabu hiyo.
![]() |
| Amepitishwa; Michael Wambura amepitishwa kugombea Urais wa Simba SC |
Amesema kila muweka pingamizi lazima awasilishe pingamizi lake kwa maandishi likiambatana na vithibitisho. “Pia pingamizi hili liwe na jina na anuani kamili la muweka pingamizi, namba ya simu pamoja na nakala ya kadi ya Simba, na nawe mwanachama hai na mwisho wa kutoa pingamizi ni Mei 22,”amesema.
Ndumbaro amesema kuwa pingamizi zitasikilizwa Mei 25 katika ukumbi wa Gymkhana, Dar es Salaam na wanaotakiwa kufika katika pingamizi hizo ni muweka na muwekewa pekee.
“Kamati itatoa maamuzi ya pingamizi Mei 27. Alisema baada ya hapo utafuata usaili wa kwa wale waliopita katika pingamizi ambao utafanyika Mei 29 katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay,”.
Ameongeza kuwa siku ya usaili wagombea wanatakiwa kufika na nakala halisi ya vyeti vyake, picha ndogo na risiti ambayo amelipia kadi yake ya uanachama kwa miaka mitatu na ambaye hatakuwa na risiti atakuwa amejitoa mwenyewe kwenye kinyang’anyiro.

.png)
0 comments:
Post a Comment