• HABARI MPYA

    Monday, May 19, 2014

    BARCA YAFANYA KUFURU, MESSI ASAINI MKATABA MPYA WA KUMPIGA RONALDO...NA YASAJILI KIPA LISILOFUNGIKA LA UJERUMANI

    HATIMAYE mshambuliaji Lionel Messi amesaini Mkataba mpya Barcelona ambao unamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani, akimpiku Mwanasoka Bora wa Dunia kwa sasa, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
    Pamoja na hayo, Barcelona imetangaza kumsajili kipa wa gharama kubwa, Mjerumani Marc-Andre Ter Stegen kutoka Borussia Monchengladbach.
    Barca imeamua kujiimarisha baada ya kumaliza msimu vibaya bila taji chini ya kocha Martino, ikitolewa katika Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya na Atletico Madrid ambao pia waliwazidi kete katika mbio za ubingwa wa La Liga siku ya mwisho.
    Nyuso za furaha: Lionel Messi akisaini Mkataba mpya na Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu
    Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari Hispania, Messi atakuwa analipwa mshahara wa rekodi mpya duniani ya Pauni Milioni 16.3 kwa mwaka na amejifunga na klabu hiyo hadi mwaka 2018.
    Messi amefunga mabao 28 katika mechi 31 za ligi msimu huu alizoichezea Barca ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye Primera Division na jumla amefunga mabao 41 katika mashindano yote msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA YAFANYA KUFURU, MESSI ASAINI MKATABA MPYA WA KUMPIGA RONALDO...NA YASAJILI KIPA LISILOFUNGIKA LA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top