• HABARI MPYA

  Saturday, May 05, 2018

  SINGIDA UNITED YAJIPIGIA 4-0 KWA NJOMBE MJI FC, PRISONS YAWABWAGA LIPULI SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, SINGIDA
  TIMU ya Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Njombe Mji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Namfua, Singida.
  Ushindi wa leo umetokana na mabao ya Kambale Salita dakika ya 42, Miraj Juma dakika ya 60 kwa penalti, Lubinda Mundia dakika ya 62 na Nizar Khalfan dakika ya 90.
  Na kwa ushindi huo, Singida United inafikisha pointi 41 baada ya kucheza mechi 27 ingawa inaendelea kukamata nafasi ya tano, nyuma ya Tanzania Prisons pointi 41, Yanga 48, Azam FC 49 na Simba SC 62.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Laurian Mpalile dakika ya tisa limeipa ushindi wa 1-0 Tanzania Prisons dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa  Sokoine mjini Mbeya.  
  Ligi Kuu itaendelea kesho kwa michezo minne, Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wenyeji Maji Maji wataikaribisha Mtibwa Sugar, Kagera Sugar FC wataikaribisha Mbeya City FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Stand United FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga na Simba SC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA UNITED YAJIPIGIA 4-0 KWA NJOMBE MJI FC, PRISONS YAWABWAGA LIPULI SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top