• HABARI MPYA

    Thursday, May 03, 2018

    SIMBA SC YAITISHA MKUTANO WA MABADILIKO YA KATIBA MEI 20 MWALIMU NYERERE

    Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa klabu ya Simba SC umeitisha Mkutano wa mabadiliko ya Katiba utakaofanyika Mei 20, mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo eneo la Ocean Road mjini Dar es Salaam.
    Mkutano huo umeitishwa na Kaimu Mwenyekiti, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye amesema kwamba utaanza Saa 3:00 asubuhi na siku chache zijazo wanachama wataumiwa ajenda kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya klabu hiyo, kufungu cha nne.
    Mkutano huo utafuatia ule wa Desemba 3, mwaka jana, ambao uliazimia kumfanya mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji kuwa mwanahisa mkuu wa klabu katika mfumo mpya wa uendeshwaji wa Simba SC.
    Mo pekee aliweka dau la Sh Bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa Sh. Bilioni 20 miezi miwili iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja.
    Wanachama 1320 walihudhuria mkutano huo wa Desemba kutoka Dar es Salaam na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji alitoa ahadi 10 za kuleta mabadiliko makubwa, ikiwemo ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa nyasi za asili na nyasi bandia pamoja na hosteli ya kisasa ya wachezaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAITISHA MKUTANO WA MABADILIKO YA KATIBA MEI 20 MWALIMU NYERERE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top