• HABARI MPYA

  Sunday, May 06, 2018

  SIMBA SC YA POPADIC WATU WALIKUWA WANASTAREHE KWA SOKA SAFI NA USHINDI MNONO

  Kocha wa Simba SC, Mserbia Dragan Popadic akizungumza na kiungo aliyekuwa anaweza kucheza kama beki pia, Mwanamtwa Mussa Kihwelo kabla ya moja ya mechi za timu hiyo mwaka 1995 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru mjini Dar es Salaam 
  Popadic aliiwezesha Simba kutwaa mataji saba kati ya mwaka 1994 na 1996, mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame miaka 1995 na 1996, ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, 1994 na 1995, ubingwa wa Ligi ya Muungano mwaka 1994 na ubingwa wa Kombe la Nyerere miaka ya 1994 na 1995.
  Popadic aliingia Simba akichukua nafasi ya kocha mzawa, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ aliyekuwa akisaidiwa na Mhabeshi, Entenneh Eshenteh ambao kwa pamoja waliifikisha timu hiyo Fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YA POPADIC WATU WALIKUWA WANASTAREHE KWA SOKA SAFI NA USHINDI MNONO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top